SHINDANO LA MASOKO WANAFUNZI ELIMU YA JUU LAZINDULIWA

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imezindua Shindano la Masoko ya Mitaji kwa Wanafunzi wa vyuo Vikuu pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka 2019 ikiwa ni mkakati wa kuwajengea uwezo katika eneo la masoko ya mitaji.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama akifafanua zaidi wakati wa uzinduzi wa shindano hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam amesema mbali ya kuwajengea uwezo pia litasaidia kuifanya sekta hiyo kutambulika na watanzania walio wengi.
“Uzinduzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mamlaka wa miaka mitano 2018/2019 hadi 2020/ 2023 ikwa ni dhamira ya Serikali kuendeleza sekta ya Masoko na Mitaji kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali.
“Mkakati mwingine ni kuongeza uelewa na ushiriki katika Masoko ya Mitaji kwa lengo la kupanua wigo kwa washiriki hao kujenga uwezo wa watendaji katika sekta hiyo,amesema.
Ameongeza kwamba mamlaka hiyo inatekeleza mikakati kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma na kwa makundi mengine akiwemo Shindano kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini.

Na kwamba Wawekezaji na washiriki katika shindano katika Masoko ya Mitaji wanahitaji kupata uelewa wa kutosha kuhusu Masoko ya Mitaji na namna ya kushiriki hatua umuhimu ya kuwawezesha kulinda maslahi yao na kufanya uwekezaji huo kuwa endelevu.
“Ukweli ni kwamba elimu kuhusu Masoko ya Mitaji itawawezesha pia kundi la Wanafunzi kuepuka kushiriki fursa za uwekezaji za kitapeli na udanganyifu,”amesema.
Pamoja na mambo mengine Mkama amesema kuwa tangu kuanza kwam ashindano hayo kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa wanafunzi wa Vyuo kushiriki na kuongezeka mwaka 2015/2016 washiriki walitakiwa kuwa 2000 lakini waliopatikana walikuwa washiriki 7,500 na 2016/2017 lengo ilikuwa 7000 wakapata washiriki 7,901,2017/2018 lengo lake ilikuwa 10,000 wakapata 15,004.
Wakati mwaka huu ilikuwa ni kupata washiriki 16,000.
Kuhusu washindi Mkama amesema watapelekwa katika nchi mbalimbali katika kujifunza namna wanavyoendesha sekta hiyo na kwamba wanaamini washiriki kwenye shindano hilo watakuwa wamepata fursa ya kujenga uwezo mkubwa katika kuielewa sekta hiyo.
Na Mwandishi Wetu


Comments are closed.