The House of Favourite Newspapers

SHINDANO YA VIPAJI DUCE: ‘INJINIA SOOOMA HIYOOO!”

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kampasi ya DUCE, wakishiriki maonyesho ya kipaji cha kucheza.

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kampasi ya DUCE, wikiendi iliyopita walifanya tamasha la nguvu la kuonyesha vipaji mbalimbali ikiwemo mitindo ya mavazi, uchoraji, kucheza, kuimba na mambo mengine. 

 

Mwanamitindo akifanya yake jukwaani.

Tamasha hilo na aina yake limeacha gumzo kutokana na vipaji bora walivyoonyesha vijana hao huku burudani ikitikisa na wanafunzi wakijiachia kwa kucheza na kuburudika.

 

Vipaji vya kudansi vilikuwa ‘balaa’.

Tamasha hilo lilifanyika kwenye kampasi hiyo iliyopo Chang’ombe jijini Dar na kuhudhuriwa watu mbalimbali akiwemo mkufunzi wa ujasiriamali, James Mwang’amba,  mwanamuziki Whozu mkali wa kibao cha ‘Huendi Mbinguni’ na wengine kibao.

Waziri wa michezo wa chuo hicho (mwenye kofia) akifuatilia onyesho hilo kwa umakini.

Moja ya matukio ambayo yaliwaacha watu midomo wazi ni baada ya mwanafunzi ambaye pia ni msanii wa uchoraji kuibuka na picha ambayo alimchora Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri,  ambaye amekuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kauli zake za kuhamasisha maendeleo ambazo wengine huzichukulia kama utani.  Mfano  ni kauli ya ‘Injinia soooma hiyoooo!‘ aliyoitumia wakati akikagua ujenzi wa moja ya majengo mkoani humo.

 

‘Soooma hiyooo…’  huyu akionesha kipaji cha kuchora.

Sambamba na tamasha hilo Mkufunzi wa Ujasiriamali, James Mwang’amba, naye aliwapa somo la ujasiriamali wanachuo hao ambalo lilivuta hisia zao kwa kiwango kikubwa.

Taswira ilivyokuwa ukumbini. 

Pamoja na hayo pia palizulinduliwa APP ya Global Publishers chuoni hapo ambapo wanafunzi hao walishauriwa kujiunga na APP hiyo ili wawe wa kwanza kupata matukio mbalimbali yanayojiri  nchini na ulimwenguni, usaili wa mastaa, burudani, michezo, vitabu vya mhamasishaji na mjasiriamali  Eric Shigongo,  katika mfumo wa maandishi (text) na sauti (audio).

Ni umakini mtupu ulivyokuwa ukumbini. 

Akizungumza na wanachuo hao, mwakilishi wa Global Publishers, Snash Sekidia, aliwaambia wanafunzi wajiunge na APP hiyo ili kuwa miongoni mwa wafuatiliaji zaidi ya milioni tatu wanaoifuatilia Global APP kila siku ambapo Jumatatu ijayo, litaanza shindano ambalo kwa wanaopakua Global App watajishindia ‘tablets’ na ‘bundles’ za Internet.

Baadhi ya washiriki wakiwa jukwaani kusubiri mchujo.

 

Mwakilishi wa Global Publishers, Snash Sekidia,  akiwaeleza wanachuo umuhimu wa kuwa na APP ya Global Publishers wakati akiizindua APP hiyo chuoni hapo.

 

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL    

Wanachuo DUCE Washindana Kuonesha Vipaji, Global APP Yatikisa

Comments are closed.