Shinikizo la Damu (Hypertension)-3

hypertension2Leo nitaelezea  mambo yanayosababisha shinikizo la damu ili uyafahamu na kujihadhari nayo.

MaMBO hayo ni uvutaji sigara, unene (visceral obesity) yaani unene wa sehemu za tumbo, unywaji pombe, upungufu wa madini ya potassium, upungufu wa vitamin D, kurithi, umri mkubwa, chumvi na madini ya sodium kwa ujumla, ongezeko la kemikali kwenye figo (renin) na kushindwa kufanya kazi kichocheo cha Insulin.

Aina ya pili ya shinikizo la damu husababishwa na tatizo lililopo mwilini. Matatizo hayo ni pamoja na kasoro ya kuzaliwa nayo katika mshipa mkubwa wa damu, saratani ya figo, saratani ya tezi iliyo juu ya figo, hali ya kushindwa kupumua vyema usingizini (sleep Apnea), ujauzito ambapo baadhi ya wajawazito hupata shinikizo la damu suala linalosababisha hatari ya kupata kifafa cha mimba (eclampsia).

Pia magonjwa ya figo kama vile mshipa wa damu wa figo kuwa mwembamba yaani Renal Artery Stenosis, matumizi ya baadhi ya dawa, kama dawa za kulevya au kemikali na kadhalika.

DALILI ZAKE

Mgonjwa anaweza kuhisi hali zifuatazo. Uchovu, maumivu ya kichwa, mapigo ya moyo kwenda mbio, kichefuchefu, kutapika, damu kutoka puani, kutoona vizuri (blurred vision), kupauka kwa ngozi au kuongezeka wekundu wa ngozi, kuhisi hali ya woga, kusikia kelele masikioni na mara chache kuchanganyikiwa.

Pale mtu anapokuwa na dalili za shinikizo la damu hupaswa kufanyiwa uchunguzi na vipimo vifuatavyo ili kuhakikisha kwamba ana tatizo hilo.

Ni muhimu kupimwa shinikizo la damu mara kwa mara (angalau mara moja kila baada ya mwaka mmoja au miwili). Unashauriwa kutokunywa vinywaji vyenye kafeini au kuvuta sigara kabla ya kupimwa shinikizo la damu.

Tukutane wiki ijayo kwenye gazeti hili hili.


Loading...

Toa comment