Shinikizo la Damu (Hypertension) – 5

Causes-hypertension-info-550x455Leo nitamalizia sehemu ya mwisho ya makala yetu kwa kutoa ushauri nini cha kufanya ili kukabiliana na tatizo la shinikizo la damu pia ufahamu na matibabu yake.

USHAURI

Mbali na kutumia dawa tulizozitaja, tunashauri kuwa  tunaweza kuzuia na kudhibiti shinikizo la damu kwa njia tofauti ambazo ni:

1). Kula lishe bora na chakula kusichokuwa na mafuta mengi, na pia chenye madini ya potassium kitaalam kinaitwa DASH diet ambacho ni maalum kwa ajili ya kuzuia shinikizo la damu.

2). Kufanya mazoezi mara kwa mara, angalau nusu saa kwa siku.

3). Kuacha kuvuta sigara na kunywa pombe kwa wale wenye tabia hizo.

4). Kupunguza utumiaji wa chumvi nyingi katika chakula hasa ya kuongezea mezani (tunapaswa kutotumia zaidi ya gramu 1.5 ya chumvi kwa siku).

5). Kupunguza msongo wa mawazo na kuhakikisha kuwa tunakuwa na uzito unaotakiwa kiafya kulingana na kimo, na kama tuna uzito uliozidi tunapaswa kupunguza uzito huo ili uwe katika kiwango kinachotakiwa.

6). Kula samaki au kutumia mafuta ya samaki ambayo husaidia kupunguza shinikizo la damu, kwa wenye shinikizo la damu.
Toa comment