BAHATI ya utajiri imemdondokea mchimbaji mdogo wa madini, Joseph Temba, baada ya hivi karibuni kuuza almasi yake yenye karati 512 kwa takriban dola milioni moja nukta nne sawa na Tsh. Bilioni 3.
Temba alipata alamasi hizo katika eneo la Maganzo mkoani Shinyanga ambapo ameishukuru Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa muongozo na usimamizi wa almasi yake na muongozo wa utaratibu wa mauzo ambao ulikuwa wazi na kutoa wito kwa wachimbaji wadogo wenzake kufuata utaratibu uliowekwa na serikali kwani kuna faida nyingi, hivyo hawana sababu ya kukwepa masoko hayo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanlaus Nyongo, alisema almasi hiyo ndiyo kubwa zaidi kuwahi kupatikana Tanzania na akaongeza kwamba serikali imejipatia shilingi milioni 238 kutokana na mauzo ya madini hayo.
Nyongo amewahimiza na kuwasisitizia wachimbaji na wanunuzi kote nchini kufanya shughuli hizo kwenye masoko ya madini yaliyoainishwa na kutambuliwa na serikali.
Aidha, amempongeza Temba kwa kufuata utaratibu katika mauzo yake na kwamba serikali itaendelea kusimamia mauzo yake mpaka hatua ya mwisho.
Hatua hiyo inajiri miezi minane baada ya almasi ya zaidi ya karati 700 kupatikana ambayo ni kabwa zaidi kuwahi kupatikana nchini Sierra Leone kwa nusu karne.
Comments are closed.