The House of Favourite Newspapers

Shinyanga: Mfanyakazi TTCL Afariki kwa Kupigwa Jiwe na Mumewe

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Alchelaus Mutalemwa.

MFANYAKAZI wa shsirika la simu nchini (TTCL) mkoani wa Shinyanga aitwaye Bupe Jacob maarufu kwa jina la Mwakibibi (48) ameuawa kwa kupigwa jiwe kichwani na mume wake aitwaye Shyrock Kimaro (48) mwendesha bodaboda mkazi wa Ibadakuli mjini Shinyanga. fb_img_1541511268309-jpeg.923932

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Alchelaus Mutalemwa,  tukio hilo limetokea Novemba 5, 2018 majira ya saa 12 jioni katika Mtaa wa Miti Mirefu, Kata ya Mjini, Manispaa  

ya Shinyanga.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi baina ya Shyrock na mkewe Bupe ambao walitengana hivi karibuni.

“Siku ya tukio Bupe alimpigia simu mme wake akiomba pesa za matumizi ya mtoto lakini katika kutoelewana walianza  kujibizana na kusukumana ambapo Bupe akaanguka chini.  Mme aliyekuwa amelewa akachukua jiwe na kumpiga mkewe kichwani akafariki dunia,” amesema Kamanda Mutalemwa akiongeza polisi inamshikilia mtuhumiwa na atafikishwa mahakamani.

 

 

Comments are closed.