Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja amefariki dunia papo hapo baada ya kukanyagwa na gari wakati dereva akirudisha gari lake nyuma bila kuchukua tahadhari.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo nyumbani kwao na mtoto huyo katika Mtaa wa Mabambasi, Kata ya Ndembezi, Manispaa ya Shinyanga.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa huo, David Nkulila amesema mtoto huyo amekanyagwa na gari hilo linalodaiwa kuwa ni la serikali.