The House of Favourite Newspapers

Shirika la Ndege la Afrika Kusini Lafilisika

0

SHIRIKA la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways) limesitisha jumla ya safari zake 38 za ndani na nje ya nchi wiki hii, ikiwa ni juhudi za kujikwamua kutokana na matatizo ya kifedha yanayolikumba. Miongoni mwa safari hizo ni pamoja na zile za Johannesburgh, Cape Town, Durban na mji wa Munich Ujerumani.

 

Shirika hilo limefilisika na kukumbwa na uhaba mkubwa wa fedha baada ya serikali ya Afrika Kusini kushindwa kutoa dola milioni 137 kutoka kwenye mfuko wa dharura ili kulisaidia  wakati lilipopata matatizo ya kifedha Desemba 2019.

Shirika hilo ambalo liko chini ya umiliki wa serikali ya Afrika Kusini  na kampuni ya nishati ya Eskom, limekumbwa na msukosuko wa kifedha kwa karibu muongo sasa kutokana na usimamizi mbaya. Matatizo ya kifedha kwa kampuni zinaziomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini yanaonekana kutishia uchumi wa Afrika Kusini hivi sasa.

 

Leave A Reply