The House of Favourite Newspapers

Shirika la Ndege la Etihad Lang’ara Tena Tuzo za Ubora Duniani

wta-5363

Makamu wa Rais wa ShirIka la Ndege la Etihad, Kitengo cha Huduma kwa Wateja Linda Celestino na Meneja Masoko na Mawasiliano Abdulrahman Al-Hadhrami, wakipokea tuzo za ‘World’s Leading Airline’ na ‘World’s Leading Airline – First Class’ wakati wa sherehe za 23 za utoaji tuzo hizo zilizofanyika Maldives.

Shirika la Ndege la Etihad kwa mara nyingine limenyakua tuzo ya watoa huduma bora wa kwanza zilizotolewa kwa mara ya 23 na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) katika sherehe zilizofanyika mwaka huu.

Ushindi huo umelifanya Shirika hilo kufikisha tuzo nane kwa mwaka huu ambazo limezipata kutoka kwa taasisi zinazoheshimika ulimwenguni. Sherehe za kukabidhiwa tuzo hizo zilifanyika kwenye ufukwe wa Sun Siyam Iru Fushi katika visiwa vya Maldives.

Shirika hili la ndege la Etihad pia lilipokea tuzo ya kuwa watoa huduma bora kwa daraja la kwanza na ukarimu unaotolewa kwa kiwango cha hali ya juu ikiwa ni pamoja na kupigiwa kura kutokana na kuwa na machapisho bora, ushauri na huduma bora zaidi kwa wateja.

Tuzo za The World Travel zinajumuisha idadi kubwa ya wapiga kura waliopo katika sekta ya usafirishaji pamoja na watu wengine kutoka kwenye jamii wapatao wapigakura 1.2 kwenye Grand Tour 2016.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad alisema, “Dhamira yetu ni kuandaa sera na kuleta mabadiliko kwenye sekta ya usafirishaji wa anga ili iendelee kutambuliwa na kupata tuzo kila mwaka. Tunajivunia kwa mara nyingine tena kwa kupata tuzo hizi mbili za heshima kwa kile tunachoamini kuwa watoa huduma bora na wenye uzoefu kwenye sekta ya usafiri wa anga.”

Tuzo za The World Travel ni jambo la msingi ambapo imewezesha kuonyesha mafanikio ya shirika letu la ndege la Etihad na kuleta mabadiliko Abu Dhab ambako ndiyo makao makuu ya shirika hili na kuufanya mji huo kuwa kitovu cha kibiashara na utamaduni ulimwenguni kote.

Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa shirika hili la ndege kupokea tuzo mbalimbali za ubora na huduma. Ndani ya mwaka huu tuzo kadhaa zimenyakuliwa zikiwamo ubora wa daraja la kwanza, na nyingine ya hivi karibuni ya utoaji huduma bora Mashariki ya Kati na huduma bora za mapumziko kwenye uwanja wa ndege katika ukanda huo.

Rais wa Tuzo za World Travel, Graham Cooke alisema, “Kwa mara nyingine tena Shirika la Ndege la Etihad limekuwa kinara kwenye sekta ya usafiri wa anga.

Wapigakura wa tuzo za World Travel hujumuisha wadau waliopo kwenye sekta ya anga pamoja na umma wa watu wengine, ambao wametambua mchango wa shirika hili kwenye usafiri wa anga na kujizolea tuzo. Bila shaka shirika hili lilistahili kupokea heshima hii.”

“Salamu zangu za pongezi nazielekeza kwa timu ya wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Etihad kwa kupata mafanikio haya makubwa na ninatumaini huu ni mwanzo wa kujiandaa na Grand Tour 2017,” Alisema.

Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad

Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad (EAG) linafanya shughuli zake ulimwenguni kote likifanya biashara kupitia mashirika yake manne ambayo ni; Shirika la Ndege la Etihad, The National Airline of The United Arab Emirates, Etihad Engineering, Hala Group na Airline Equity Partners.

Shirika limewekeza kwenye mashirika saba mengine ambayo; Airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia na Swiss-based Darwin Airline, inayofanya kazi chini ya Etihad.

Shirika la Etihad lenye makao makuu yake Abu Dhab limejiwekea malengo ya kuhudumia abiria na usafirishaji mizigo maeneo zaidi ya 110 na kutoa huduma bora ya usafirishaji mizigo Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Amerika.

Shirika lina ndege za Airbus na Boing 120, ikiwa na zingine 204 ambazo bado zinatumika kwa sasa; ikiwamo 71 Boeing 787s, 25 Boeing 777Xs, 62 Airbus A350s na 10 Airbus A380s.

Kwa maelezo zaidi tembelea: www.etihad.com

Kwa mawasiliano zaidi:
James Sanderson
Shirika la Ndege la Etihad
Simu: + 971 2 511 3657
Baruapepe: [email protected]

Comments are closed.