The House of Favourite Newspapers

Shirika la Ndege la Etihad Lapanua Huduma Zake Ulaya          

etihad-cargo-boeing-77f

Ndege ya mizigo ya  Shirika la Ndege la Etihad, Boeing 777 kupitia kitengo chake cha Etihad Cargo.

Idara ya Usafirishaji Mizigo ya Shirika la Ndege la Etihad, imeanzisha ndege tatu kwa ajili ya kuimarisha sekta ya usafirishaji bidhaa barani Ulaya.

Mwezi uliopita kitengo hicho kilianzisha ndege ya Boeing 777 kutoka East Midlands na Uwanja wa Ndege wa Stansted nchini Uingereza na kutokea Copenhagen nchini Denmark.

Makamu wa Rais, wa Idara ya Usafirishaji Mizigo ya Etihad, David Kerry alisema, ”Tumetekeleza mahitaji ya wateja wetu kulingana na umuhimu wa usafirishaji nje ya Ulaya, pia ndege zetu zina uwezo wa kutoa huduma kulingana na mazingira yaliyopo pindi inapohitajika.”

Alisema, “Huduma hizi mpya zitawaunganisha wazalishaji na wateja karibu ulimwenguni kote. Wazalishaji nchini Uingereza na Denmark sasa wanaweza kukutana na wateja wao waliopo Mashariki ya Kati kwa haraka zaidi ndani ya masaa 24.”                                                                                                           

Mwendeshaji Mkuu wa Copenhagen Airport, Peter Krogsgaard alisema,” Tunayofuraha kwa Kitengo cha Usafirishaji cha Etihad Cargo kuanzisha shughuli zake katika Uwanja wa Ndege wa Copenhagen. Usafirishaji mizigo kwa njia ya anga ni muhimu zaidi kwa ukuaji wa haraka kibiashara kwa Wadenmark.

Asilimia kubwa ya Wadenmark hutumia zaidi huduma za usafirishaji kwa njia ya anga ambao pia wengi wao ni ndege. Copenhagen ni kitovu muhimu cha biashara kwa Ukanda wa Ulaya Kaskazini kwa usafirishaji wa mizigo kwa njia ya anga na kimataifa kutokana na uwekezaji uliofanywa na Shirika la Ndege la Etihad katika kuimarisha soko la kimataifa.”

Safari hizi mpya zimewezesha kufikia tisa kwa ndege zinazofanya safari zake Ulaya. Tayari Kitengo cha Usafririshaji cha Etihad kimeifikia miji mingine Ulaya kama vile Amsterdam, Frankfurt (Frankfurt Main na Frankfurt-Hahn), Milan, Brussels pamoja na Zaragoza ikiwamo na huduma za usafiri wa anga kwa abiria katika maeneo mbalimbali barani Ulaya.

Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa washirika muhimu wa kibiashara na Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu ambapo inakadiriwa biashara ya mafuta ya zaidi ya dola 65 za Marekani ilifanyika mwaka 2015. Kwa mwaka huo huo Nchi za Falme za Kiarabu ilikuwa miongoni mwa nchi kubwa ikishika nafasi ya nane  inayofanya biashara na Ulaya huku Umoja wa Ulaya ikiwa ya 13 kwa kufanya biashara kimataifa kwa ujumla.

Kuhusu Shirika la Ndege la  Etihad

Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad (EAG) linafanya shughuli zake ulimwenguni kote likifanya biashara kupitia mashirika yake manne ambayo ni; Shirika la Ndege la Etihad, The National Airline of The United Arab Emirates, Etihad Engineering, Hala Group na Airline Equity Partners.

Shirika limewekeza kwenye mashirika saba mengine ambayo ni; Airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia na Swiss-based Darwin Airline, inayofanya kazi chini ya Etihad. 

Shirika la Etihad lenye makao makuu yake Abu Dhabi limejiwekea malengo ya kuhudumia abiria  na usafirishaji mizigo maeneo zaidi ya  110 na kutoa huduma bora ya usafirishaji mizigo Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Amerika. Shirika lina ndege za Airbus na Boeing 120, ikiwa na zingine 204 ambazo bado zinatumika kwa sasa;  ikiwamo  71 Boeing 787s, 25 Boeing 777Xs, 62 Airbus A350s na 10 Airbus A380s.

 

Kwa maelezo zaidi tembelea: www.etihad.com

Kwa mawasiliano zaidi:

Siobhan Bardet

Shirika la Ndege la Etihad

Simu: + 971 2 511 1049

Baruapepe:   [email protected]

Comments are closed.