The House of Favourite Newspapers

Shirika la ndege la Etihad latajwa kuwa shirika bora la ndege, baada ya kunyakua tuzo ya sekta ya usafiri wa anga New Zealand

taanz-awards_etihad-airways-team-at-award-ceremony

Meneja Mkuu wa Etihad nchini Australia na New Zealand, Sarah Built akiwa na tuzo pamoja na wadau mbalimbali wa shirika hilo.

Shirika la ndege la Etihad limetajwa kuwa Shirika bora la Kimataifa katika tuzo za Chama cha Mawakala wa Safari cha New Zealand (TAANZ) zilizotolewa mjini Auckland, Septemba 10 mwaka huu.

Kutokana na kura zilizopigwa na Sekta ya Usafirishaji New Zealand, tuzo hiyo imelipitisha shirika hilo kuwa na ubora wa bidhaa na huduma za anga duniani.

Meneja Mkuu wa Etihad nchini Australia na New Zealand, Sarah Built ambaye alipokea tuzo hiyo, kwa niaba ya Etihad alisema: “Ningependa kuwashukuru washirika wetu wa usafirishaji nchini New Zealand kwa kutupigia kura za kutuamini na kuendelea kutuunga mkono.Pia, niishukuru timu ya mawakala wetu wa mauzo waliopo New Zealand kwa juhudi zao endelevu za kuiwakilisha Etihad katika masoko.

Bi. Built aliwapongeza wanahisa wa Etihad, Virgin Australia na washirika wake New Zealand kwa mchango wao katika mafanikio ya Etihad.

Tukiwa pia kama watoaji wa huduma zingine tofauti na za anga nchini New Zealand, tunategemea nguvu za washirika wetu ili kutoa huduma zisizo na mipaka zitakazounganisha Tasman na maingilio ya Australia. Ushirika wetu na Mashirika haya ni muhimu kwa maendeleo ya soko letu nchini New Zealand.

Etihad inashirikiana na Virgin Australia na Air New Zealand kwa safari za kutoka Auckland, Christchurch, Queenstown na Wellington kwenda vituo vinne vya Brisbane, Sydney, Melbourne na Perth katika maingilio ya Australia.

Huu ni Mwaka wa tatu tangu tuzo za mwaka za TAANZ kuanza kutolewa, huku ikiwa ni tuzo ya kwanza kwa  Shirika la Etihad katika kategoria ya huduma za usafirishaji.

Comments are closed.