The House of Favourite Newspapers

Shkuba Mikononi mwa Trump

0

STORI: MWANDISHI WETU | GAZETI LA UWAZI |  DAR ES SALAAM

Ofisi ya Waziri wa Katiba na Sheria, imewasilisha maombi ya kuwasafirisha washitakiwa watatu akiwemo Ally Hatibu Hassan maarufu kama Shkuba kwenda nchini Marekani inayoogozwa na Rais Donald Trump kwa ajili ya kujibu tuhuma za kusafirishaji madawa ya kulevya

Washitakiwa wengine ambao wanaungana na Shkuba ni Idd Mafuru na Lwitiko Emmanuel Adam.

Watuhumiwa, Shkuba na Tiko

Maombi hayo yamewasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya kifungu namba 5 (1) cha Sheria ya Usafirishaji wahalifu sura ya 368 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Rais wa Marekani, Donald John Trump

Katika maombi hayo upande wa waziri kupitia Mkurugenzi wa Mshitaka (DPP) wanaiomba mahakama hiyo isikilize ushahidi na itoe amri ya kuwahifadhi washitakiwa ndani wakiwa wanasubiri kibali cha waziri huyo cha kuwasafirisha nje ya nchi kwa mashitaka hayo.

Kwa kuwa Shkuba anashikiliwa gerezani Lindi, gazeti hili lilimpigia simu Kamishna Mkuu wa Magereza, Dk. Juma Malewa na kumuuliza kuhusu habari hiyo naye akajibu kwamba hana taarifa hiyo. Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi hakupatikana.

 

 

Leave A Reply