The House of Favourite Newspapers

Shoga; chakula hakiliwi kwa kufunikwa!

0

Couple-in-BedNAAM ni siku nyingine tena tumekutana katika kona yetu hii. Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema natumai na nyinyi ni wazima ila kwa wale wagonjwa niwaombee mtapona.

Wiki iliyopita niliwaletea mada ya wale mashoga zangu wenye midomo ya bata, wale ambao wakiona maji kidogo wao kunywa tu. Usitoe macho! Namaanisha wale wapenda kuropoka ambao hawatunzi siri ya chakula cha usiku, upo!

Baada ya hayo, tugeukie kwenye mada yetu ya wiki hii shoga. Nianze kwa kukuuliza shoga yangu, hivi unawezaje kula chakula kilichofunikiwa? Utakuta chakula umekiandaa vizuri, mboga safi tena vijana wa sasa wanaita mboga saba na ni kitamu hasa lakini unataka kiliwe kikiwa kimefunikwa, ina hu?

Nikung’ate tu sikio shoga, ukitaka ukifurahie chakula cha usiku, kwanza hakikisha unakiandaa vizuri yaani mnashirikiana katika kukiandaa, mwenzako akileta kisu basi mpe vitunguu ama nyanya akate, akiweka mafuta basi tia mboga kisha mshirikiane katika kukitengeneza baada ya hapo chukua mwiko na muanze kusonga pamoja, upo?

Sasa pamoja na kushirikiana kote huko bado shoga wewe unataka kukila eti kiwe kimefunikwa, loh! Wee naweee!! Utajuaje sasa kile chakula mlichoshirikiana kukipika kwa mbwembwe zote tena huku mkirushiana mikono na miguu hutaki akione hadi pale utakapojisikia umeshiba, ukiachwa unaanza kujuta, ohh! Huna bahati! Bahati unayo ila umeipoteza mwenyewe.

Nilishawahi kuongelea kuhusiana na ‘singlendi’ kuwa nayo ni nguo ya ndani shoga wala usikubali mwenzako alale nayo, basi kama umeifanyia kazi hata na hii ya chakula cha usiku nacho hakiliwi kwa kufunika.

Kama ulikuwa hujui, andika pembeni ya kwapa shoga! Ukitaka umkoleze akolezeke, umlegeze agelezeke, umchawie achawizike! Basi akirudi tu kutoka katika shughuli zake, badilika. Kama ulikuwa umekereka basi jioneshe mwenye furaha, mnyenyekee! Ukifika ule muda wa chakula cha usiku, muwashie taa kabisa afurahi, hakikisha anajiandaa kwa kupika na usiruhusu aingie uwanjani hata na ‘singlendi’, upo?

Pika naye kwenye mwanga mweupe ili ukiweka chumvi ama pilipili nyingi iwe rahisi kutambua. Mkishaandaa chakula basi kiandaliwe kukiwa na mwanga huohuo mliokuwa nao katika kukipika. Ukifanya hivyo kwa kila chakula, utaona mwenyewe raha ya hicho chakula!

Wengine wanadanganya, utasikia, ohh! Naogopa watoto! Mara tena ohh chukua ungo ufunike na hiyo ni kila ukitaka kula chakula. Mwingine hadi asubuhi anang’ang’ana kujifunika kwa ungo tena anataka kila mmoja awe na ungo wake wa kujifunika. Sasa shoga mtakulaje kikiwa kimefunikiwa wakati mmekipika wote?

Kwa leo niishie hapa! Kama una lolote la kujifunza shoga, nitumie meseji kwenye namba yangu hapo juu!

Leave A Reply