Shoga; chakula ni siri yako na mumeo!

Couple-in-BedAwali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya njema iliyoniwezesha kuandaa hiki nilichoamua kuzungumza nawe kupitia safu yetu hii.

Wiki iliyopita nilitoa mada ya kuimba ukiwa uwanjani, mwanamke sharti ujue jinsi ya kulichezea gitaa kisawasawa, imba nyimbo zote za Mchiriku, Singeli, Bongo Fleva hadi mwenyewe atakusapoti na ndiyo raha ya shabiki. Basi kuna mashosti waliyoisoma hiyo mada mimeseji niliyotumiwa shoga yangu, kumbe wengine walikuwa wameacha kabisa kuimba uwanjani lakini wamerudishwa na ile mada.

Sasa leo shoga, acha niwape somo wale ambao wakipewa chakula harakaharaka kesho yake kukimbilia kwa jirani na kumsimulia, utasikia; ‘leo baby wangu amenilisha vijiko vingi hadi nimechoka! Ni fundi wa kulisha kweli tena kwa mikono yote’ sasa shosti unamwambia ili iweje, ina hu? Umeshamuamsha mwenzako, akaamka na kuhamasika sasa akimtamani na yeye akapewa hicho chakula na mumeo utamlaumu nani?

Wengine wanafika mbali na kusimulia udhaifu wa mumewe utasikia; ‘Yaani shoga, mume wangu hakuwa hivi, siku hizi anarudi amechoka kweli, ananipa kijiko kimoja tu anadai amechoka’ sawa amechoka, wa kukusaidia kujua kwa nini amechoka ni jirani kweli?

Shoga jifunze kutunza siri ya chakula chako na mumeo. Iwe anakulisha kwa mikono yote, iwe anashindwa kukulisha hiyo ni siri yako na yeye. Mashoga wengine wao wakikaa kama kusukana au gengeni ama kwenye makundi ya Mtandao wa WhatsApp stori zao kubwa ni kila mmoja kumuelezea mumewe utasikia; ‘Leo usiku sijalala, nimemuandalia vyakula vyote, kala akaniambia hajashiba, basi hilo sebene la uwanjani mbona kashiba mwenyewe!’ Huko kushiba vipi tena?

Wengine wakiachwa wanaanza kulaumu kumbe aliyesababisha kuachwa huko ni yeye mwenyewe. Jamani mwanamke sharti uwe msiri, iwe unafurahia chakula cha usiku ama la kausha! Hiyo ni siri yako, mshirikishe mumeo, mwambie unavyofurahia na unavyochukia pale anapokulisha.

Bibi zetu ndiyo maana walikuwa wakidumu sana kwenye ndoa zao kwani walikuwa wasiri sana. Hata wanyimwe chakula miezi na miezi huwezi kusikia cha kwa jirani wala mjumbe na kipindi hicho hakuna cha WhatsApp wala Facebook labda mkutane kisimani na huko unahesabiwa saa tu uwe umerudi. Makoo yao yaliwekewa kitu cha mgando na midomo yao haikuwa ikikaa wazi muda wote, upo shoga!

Kwa leo niishie hapa, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri!


Loading...

Toa comment