The House of Favourite Newspapers

Shoga; Kiguu Na Njia Chako Kitamkimbiza Mumeo Nyumbani!

0

loveShoga, leo ni Jumanne nyingine ambapo tunakutana katika hiki kilinge chetu tunachokitumia kupeana darasa la namna ya kuishi na familia zetu hususan waume zetu ambao tulikubali kwa ihari yetu kuungana nao na kuwa mwili mmoja.

Hata hivyo, kabla sijasonga mbele kuhusu nilichopanga kuzungumza nawe, niwasisitize mpatapo nafasi msiache kwenda kuhudhuria kwenye mikutano ya kampeni katika kipindi hiki cha lala salama kusikiliza sera za wagombea wa nafasi ya udiwani, ubunge na urais ili Oktoba 25 muwachague viongozi wanaofaa.

Baada ya kusema hayo, sasa narejea kwenye jambo nililowaandalia ambalo naamini utakuwa umejua linahusu nini kutokana na kichwa kinavyojieleza hapo juu.

Ni kweli kabisa shoga yangu, kama haupo makini na hizo safari zako zisizoisha kuna mambo mawili yatatokea, kama siyo kumkimbiza mumeo nyumbani basi atakutafutia nyumba ndogo inayojua kutulia nyumbani.

Ninaposema hivyo simaanishi muache kwenda kwenye mihangaiko ya kutafuta riziki, kuhudhuria misibani, sherehe na mambo mengine ya kijamii, la asha!

Safari ninazozizungumzia ni zile zisizo na tija, namaanisha mke wa mtu kila uchawo kwenda kwenye ngoma, kwa shoga zako au hata kwa wazazi au nduguzo bila kuwa na sababu za msingi.

Mbaya zaidi ni pale mwanamke aliyeolewa kumuacha mumewe nyumbani siku ambayo yupo off bila kujali kama atapenda kuitumia siku hiyo ya mapumziko kuwa naye chumbani zaidi.

Ukiacha kuwa naye kimalovee, wanaume wengi hupenda wanapokuwa nyumbani wale vyakula walivyopikiwa na wake zao, kuandaliwa maji ya kuoga hata kuondolewa nywele zote zilizomo mwilini mwao pamoja na kukatwa kucha.

Shoga, unafikiri ni mwanaume gani atakuwa tayari kumvumilia mwanamke ambaye kila siku yeye ni kiguu na njia kama siyo kumpa nafasi ya kutafuta mchepuko?

Kwa mwanamke ambaye hayuko makini hilo lazima atakumbana nalo kwa sababu furaha ya wanaume safi kitabia ni kuwa karibu na wake zao wakiikosa nafasi hiyo lazima watatoka nje. Bye!

Leave A Reply