Shoga; kuimba uwanjani kunaongeza upendo
Naamini wote mpo salama na kwa wale wagonjwa nawaombea Mwenyezi Mungu awape nguvu mtapona.
Wiki iliyopita nilizungumzia kuhusu wale mashoga zangu waliozoea kulala na magauni wakati wanajua fika wameolewa.
Naamini wameshafanyia kazi na kama bado shoga yangu hebu amka! Achana na kujizibaziba kama ndiyo umetoka kuchezwa ngoma leo.
Baada ya hayo, leo nimekuja na mada ambayo wengi wamekuwa wakiwachukiza waume zao. Utakuta mwanaume anaingia uwanjani, anahangaika kupiga vinanda vya aina zote sambamba na gitaa lakini mkewe hata kuimba hawezi, anakaa kibubububu!
Shoga huwezi ukaingia uwanjani kucheza muziki unaishia kukaa tu, mwanaume wako tena wa ndoa ndiyo afanye kazi yote ya kupiga gitaa, kinanda na kukuburudisha tena anajitahidi kutoa sauti nzuri na nyororo lakini mwenzangu na mimi kimya hata kiitikio tu huwezi.
Uwanjani ni sehemu kubwa sana na kila mwanamke anayekuwepo eneo hilo huwajibika kwa kuimba. Nikung’ate sikio tu shoga yangu! Wanaume wa sasa ukitaka wakupende uwanjani we waimbie tu. Unaweza ukaimba Taarab, ukiona haimuingii mbadilishie imba Mchiriku, ukiona napo bado haimuingii basi unamuimbia zile nyimbo laini za wanamuziki kama Celine Dion, Mariah Carey utaona mwenyewe anavyochanganyikiwa.
Kama ulikuwa hujui shoga yangu, wanaume wa sasa wajanja sana, hata kama amekuoa, akiona kila akiingia uwanjani hasikii ukiimba hata kiitikio tu, taratibu ataanza kujitafutia uwanja mwingine anaoona unaweza kumpa faraja ya moyo wake kwa kumuimbia nyimbo anazozitaka.
Kuna shoga zangu wengine wameingia kwenye ndoa siku chache halafu wanaanza kulalamika ‘Ohh mume wangu uwanjani simwelewi kabisa, dakika mbili tu anamaliza mechi hataki tena!’ kumbe hajui mchawi ni yeye mwenyewe ambaye kila wakiwa uwanjani anageuka bubu! Hajui kama ameshindwa kumpa nyimbo za kumfanya asichoke kucheza.
Shoga shtuka! Ukiwa uwanjani wee imba tu nyimbo zote utaona mwenyewe, kesho yake atataka tena kuingia uwanjani na kukusikia ukimuimbia.
Kwa hiyo mashoga zangu, uwanjani siyo sehemu ya kurukaruka tu, au kucheza muziki kimyakimya bali ni sehemu ya kupokezana sauti au kuimba pamoja. Kama utaona mwenzako anaimba staili za kutaja jina lako basi na wewe muoneshe mara mbili yake, imba misemo ya kimahaba ya Kiingereza na Kiswahili huku mechi ikiendelea utaona jinsi atakavyotamani msimalize kupiga shoo.