The House of Favourite Newspapers

SHOGA; Mechi Haichezwi Matopeni!

0

HEYAHEYA! Acha nicheke miye sidaiwi na mtu, kama pumzi navuta tena hewa ya bure ya nini kujibana mwenzangu, najiachia nitakavyo! Haloooo! Kama hewa ingekuwa inauzwa kama luku mbona wengi tungepumua kwa mahesabu, hili nalo neno!

 

Ushaanza kusema ohh Anti Naa nina maneno mengi kama vile mtoto aliyebemendwa, aiiih! Jamani nyonyo mbona hivyo?

 

Kwani kucheka ni kwa wenye meno tu na siye wenye magego tusicheke, tusivaibretishe mbavu zetu? Tuvumiliane basi mate yakiwarukia muone kama pafyumu au Wazungu wanaita ‘ea kondisheni’,

haloooo eeeehhh! Ushaanza maswali yako eti ohh mate ya sigara hayavumiliki? Jamani ina maana mvuta sigara hatoi udenda? Mmh! Hayo si yangu nakuachia wewe tuendelee na yetu!

 

Kama ulikuwa hujui jua sasa, mwaka huu mbona wangu, nani alikuambia kisasi cha kitu hulipwa kwa kitu? Au mmesahau mtafuta ugomvi sharti avae skini taiti au jinsi ya kubana! Hebu twende kwa kilichotufanya tukakutana hapa!

 

Mwenzenu juzi nimefuatwa wanguwangu na binti mmoja ambaye anajua shughuli yangu kisawasawa, alinimwagia mchozi wa mwendokasi shuu, nikamuuliza una nini? Si akanimwagia ya uwanjani na mumewe, mwaaa mwari likanishuka la kunishuka shuu! Alisema ni mumewe kukosa uaminifu ndani ya ndoa yao, pili kushindwa kupatiwa mechi inayotakiwa.

 

Aliendelea kusema kuwa mume wake pamoja na kuwa naye mbali na kukutana kwa muda mchache bado amekuwa hachezi mechi kama wengine wanavyofanyiwa na wenzao na kufi kia hatua ya kila siku kuwa katika mateso, siku chache anazokuwa yupo nyumbani amekuwa akicheza mechi za matopeni, mechi za sekunde kama siyo dakika mojamoja!

 

Wazo lake kubwa lilikuwa ni kutafuta mchezaji mwingine anayefanania uwanjani kama si Messi basi Ronaldo, awe akimsaidia pale mume wake anapokuwa nje kwa kipindi cha mwezi mmoja mpaka miwili. Kwa upande wake aliona ule ndiyo ulikuwa utatuzi wa tatizo lake, lakini uamuzi ulikuwa mgumu na kuomba ushauri kabla hajafanya lolote.

 

Mmh! Mtoto wa kike ameyamwaga hadharani kwa kuwa mtu huyo wa kumtibu maradhi yake alishampata lakini alitegemea majibu yangu. Haya, mmemsikia jinsi mtoto wa kike anavyoteseka? Nikamshauri asiwe mwepesi wa kutoa uamuzi bila kuangalia hasara zake, kwani ni kubwa kuliko faida, mwanamke unapoikosa haki yako ndani katu huwezi kuitafuta nje ya ndoa.

 

Unapotokewa na tatizo la mwenzio kutokucheza vizuri uwanjani au mpenzi wako kuwa mtu wa kusafi ri kila wakati, shoga wee wee nakuomba uwe mvumilivu na kulilinda penzi lako, najua unakuwa kwenye hali mbaya, lakini ustahimilivu ni jambo la msingi sana.

 

Siku zote unapokuwa kwenye wakati kama huo, jiepushe na mawazo ya kufi kiria mapenzi au kuangalia mauchafu kwenye simu ambayo yanaweza kukupa kishawishi cha kucheza mechi. Siku zote mawazo ya mtu huelekea pale anapoyaelekeza, pia moyo una haki ya kutamani lakini wewe ndiye unayetakiwa kuuzuia. Hakika ukiuendekeza moyo utakupeleka kubaya.

 

Kitu kingine acha kuwa bubu kushindwa kumweleza ukweli mwenzako kuwa siku hizi hufurahishwi na mechi za matopeni yaani za dakika moja moja. Unatakiwa kuwa mkweli kwa mwenzako, kumueleza jinsi unavyoteseka kwa yeye kukuacha njia panda ili mtafute ufumbuzi wa tatizo lako.

Nisitiririke saaana, naomba niishie hapa! Ni mimi Anti Nasra, Shangingi Mstaafu.

Leave A Reply