The House of Favourite Newspapers

Shoga: Punda Hafi Kwa Kipigo

0

SITAKI uniulize ooh MC Sophy kazidi sasa, kila siku haanzi na salamu, kuchamba tu! Weee! Aliyekwambia hii sehemu ya kuchamba nani? Nipo hapa kutoa elimu tena likukae akilini kimbelembele we unayejikalisha na kujisemesha ukipotosha watu, loo!

Nikugeukie na wewe uliye na hamu ya kujua leo shoga yako nimekuja na nini? Punda hafi kwa kupewa kipigo! Kila siku kulalama eti ooh, mke wangu kanichoka, mchezo kiduchu kama mgao wa umeme.

Heee heeeeeiyaaaaa! Mboooona!Shoga wan’chekesha tena wan’chekesha si kiduchu sana tu! Jamani tokea lini tembo akaelemewa na mkonga wake au ukala gizani ukakosea mdomo ulipo?

 

Basi mwenzako leo nataka nikupashe upashike wewe uliyekalia mtindo mmoja wa toka ubalehe, toka uvunje ungo wa kifo sijui cha nini sijui cha paka, macho kama taa ya gari la mwendokasi! Jamani mfumo wa kuleta raha uwanjani ulibadilika kwa nini na wewe usibadilike.

Siku hizi dunia imeendelea ati, kila siku mambo yamebadilika na watu wanakwenda na wakati, zamani tulikuwa analojia sasa mambo yote dijitali au siyo jamani bila king’amuzi siku hizi huoni TV, uongo?

Mwanaume lazima uwe mbunifu basi kujua mpenzi wako anataka nini au anakosa kitu gani? Siyo umejiweka kama lori bovu likiteremka kwenye mlima.

Tena nasikia kuna baadhi ya wanawake wamezidi ubishi wakielezwa geuka hivi eti usumbufu, nani alikuambia mapenzi ni mchezo wa kujipikilisha kama watoto wanaojifunza kuongea?

 

Si naongea na  wewe unayejifanya kazi yako kumsubiri  mwenzio atue mzigo kisha ateremke mlale,  upo? Kwa taarifa yako punda hafi kwa  kipigo!

Shoga wee, uguswapo sisimka pandisha mzuka na kujituma muda wote, hakikisha uliye naye anafurahia kuwa nawe, siyo mtu anafanya ili kukamilisha zoezi. Haipendezi, raha ya kula pilipili uilalamikie ukiila, utoe mlio wa kuwashwa kila mtu ataijua kweli pilipili kali, heee heee heeeiyaaa!

Lazima niseme ukweli ati mapenzi si lelemama, usione mwanamke kanunuliwa jumba, gari mwenzako hakupata kwa njia ya mkato, kajituma shoga yangu!

Ukijua kuutumia uwanja vizuri utakuletea faida kwenye ndoa acha kuringia umbile ukadhani ndilo lililobeba ndoa. Mfyuuuuuu!

 

Leo nipo na nyie kina baba mnaojifanya kazi yenu kumwaga mzigo na kuondoka huku kila siku mtindo uleule wanaita kifo cha nini sijui mara ng’ombe kashindwa kufi ka machinjioni. Najiuliza siku ng’ombe huyo akikubali kwenda mwenyewe machinjioni itakuwaje?

Mwanaume unatakiwa uwe mtundu kwa kulianzisha kwa mpenzio kwa mazingira yoyote, usisubiri uwanjani tu na mtindo wako mmoja kama gari moshi lililoishiwa mafuta.

 

Acha kucheza mechi kwa mazoea, mwenzako alichokikuta basi hichohicho, kuna mwanamke bila kumkunja kama ndizi mbivu hajisikii raha nawe umeng’ang’ania kifo cha nini sijui basi hata ungebadili baada ya kifo uongeze na mazishi yake kabisa, halooooo ehhhh! Hilo nalo neno nyonyo!

Sitaki kuongea sana, kama una akili utanielewa shoga! Hii haiitaji uwe umesomea digirii au diploma. Tukutane tena wiki ijayo! Kwa maoni na ushauri nitumie meseji tu wala usipige, namba yangu hiyo hapo juu!

MC Sophia | UWAZI| Mapenzi & Maisha (Chumbani Zaidi)
Maoni (0713 761 135)

Tshabalala; Tumejiandaa kuifunga Yanga

Leave A Reply