The House of Favourite Newspapers

Shoga; punguza safari mumeo akuamini!

0

Namshukuru Jalali kwa kunijalia uzima ulioniwezesha kuonana nawe katika uga wetu huu tunaozungumzia ishu za chumbani zaidi.

Baada ya wiki iliyopita kuwazungumzia wenzetu wanaochepuka huku wakiwa kwenye ndoa, leo nitawazungumzia shoga zetu ambao ‘kiguu na njia’ ndiyo maisha yao.

Shoga zetu hao bila kutoka nyumbani hawawezi, mara utasikia nakwenda kwa dada Tatu Kimara, kwa shangazi Kitunda na kwenye kicheni pati Buruguni.

Kama wazazi wao wako Chanika na wao wanaishi Mbagala basi haiishi wiki bila kwenda huko, yaani wao ni safari kwa kwenda mbele na kusahau kabisa wajibu wa kutulia nyumbani.

Shoga, kwa tabia hiyo ya kila kukicha wewe ni kiguu na njia lazima mumeo atakutilia shaka na kwa ambaye hataki kupiga kelele lazima atatafuta mchepuko tu!

Atafanya hivyo kwa sababu kila akirudi nyumbani akitegemea utampokea, utampa pole ya kazi, utamwandalia maji ya kuoga na chakula, anaambulia patupu,wewe haupo.
Shoga yangu, kwa tabia hiyo ni rahisi mumeo kutokukuamini na kuhisi unamsaliti na mbaya zaidi ni pale inapotokea kila ukitoka nyumbani simu yako haipatikani hewani.

Kwa wewe mwenye tabia hiyo, unapaswa kuelewa kwamba heshima ya mwanamke ni kutulia nyumbani, hata unapotoka iwe kwa safari za muhimu lakini siyo kila kukicha wewe ni kiguu na njia.

Leave A Reply