The House of Favourite Newspapers

Shoga: Raha ya Mchezo Kushangilia

Na SOPHIA MA`MDOGO| GAZETI LA UWAZI| LOVE & LIFE

Kuna watu wakimaliza kila mmoja atachukua vyombo vyake wakati mlipoanza mmoja ndio aliandaa. Shoga mzee akimaliza kula chakula nawe sema asante chukua vyombo vyako… 

HAYA sasa shoga yangu, ni Jumanne tena mwanana tumekutana kwenye kona yetu hii ya chumbani zaidi, kona pendwa inayoongozwa kusomwa na watu wengi nchini, upo somo? Shoga hali yangu kama ulivyoniacha jana, kwa wale wenzangu na mimi tunaoishi kwenye jiji hili la Dar kidogo hali ya hewa ndiyo hivyo haitabiriki mara mvua mara jua ila kama ni mgonjwa ni jambo la kuombeana heri shoga yangu, maana ukiumwa wewe mi nakosa raha, si ndiyo? Baada ya hayo shoga langu la ukwee, kwanza nikupe mrejesho wa kile ambacho nilikiongea mara ya mwisho hapa nikakufundisha njia za kijanja, njia tano za kumfanya mzee wako ajihisi yupo ulimwengu mwingine wa maraha.

Basi somo mwenzako nilipata meseji hizo! Simu hazina idadi ndipo nikagundua kumbe wengi humu hawajui njia za kumfanya mzee akupende zaidi pindi unapokula naye chakula cha usiku.

Wengi hawajui mahabati, haaa haaa nicheke miye niongeze siku za kuishi maaana loool! Wengine wanaomba niirudie mada hiyo kwa upande wa kumpagawisha mwanamke inakuwaje, niwape njia na mautundu wakawaambie wazee wao, tisa kumi shoga yangu, wengine walilalamika kipengele cha mwisho cha kutumia kucha ningekiongeza eti niliwaacha njia panda, shoga nawe! Haya tuachane na hayo, kiporo kikiliwa zaidi ya siku tatu siyo kiporo tena.

Leo nina jipya, ninaposema jipya jipya kweli tena unisome kwa makini shoga yangu maana mimi kwa kutoa maneno yakakufika hapa! Shoga kuna kitu muhimu
unatakiwa ukifanye katika uwanja wetu, meza yetu ileee ya kula chakula cha usiku na mzee siyo mchepuko!

MASHABIKI

Shoga kwanza raha ya mechi yoyote ile lazima ichezwe kwenye uwanja safi. Hata mzee akitamani kunawa mikono mwambie asiwe na wasiwasi anawe! Siyo utakuta jitu chafu, uwanja halijui kusafisha likifunua mfuniko ili chakula kiliwe huo mchacho, loool! Baada ya kuweka uwanja safi yaani meza yako ya kula chakula cha usiku iko safi kinachofuata sasa ni mashabiki kuingia kucheza, shoga nimesema mashabiki wapo waliotoa macho, mashabiki ni wewe na mzee wako! Ingieni sasa muanze kucheza mechi, tena mechi isiyokuwa na muamuzi si unajua ilivyokuwa na raha yake, heee hee heeeiya!

KUSHANGILIA

Kama ulikuwa hujui somo wazee wa siku hizi hata kama unakula chakula kwa uchovu lakini ukijua kufunua mfuniko na chakula kikaonekana kipo safi, weee shangilia mwanzo mwisho mbona utamkamata tuu, kwanza huo mchepuko unakujaje au unatokea wapi kwa mfano? Najua kuna wengine watauliza kuna aina ngapi za kushangilia, looo! Shoga hata hilo la kuuliza! Wakati mwingine wa kujiongeza mwenyewe, ukishikwa shingoni wee shangilia, kwenye tumbo na sehemu nyingine we shangilia, upo somo?

SEMA ASANTE

Hapa sasa shoga yangu wengi wakianza kula chakula chao hushindwa kumaliza vizuri. Kuna wengine watamaliza hawajaridhika, wengine watadai wamechoka wamewahi lakini jamani neno asante ni muhimu bila kujali mzee au wewe ndiyo aseme! Kuna wengine wao hilo siyo jambo la kuwaacha, hata wamalize kula chakula sahani ya kwanza, kabla hakijaongezwa chakula kingine wale atasema asante. Akiwa katikati shangilia yake ni kusema asante.

KUCHUKUA VYOMBO

Shoga kitu cha mwisho ambacho ningependa uzingatie kwa mzee wako ni kuhakikisha mkimaliza kula tu chakula cha usiku safisha meza vizuri kisha chukua vyombo na usafishe. Nikisema hivi namaanisha somo! Kuna watu wakimaliza kula kila mmoja atachukua vyombo vyake wakati mlipoanza mmoja ndiyo aliandaa. Shoga mzee akimaliza kula chakula nawe sema asante chukua vyombo alivyotumia kula chakula na uvioshe ili viwe safi.

Comments are closed.