Shoga: Shepu yako nzuri, basi mridhishe mumeo!

tinayamout2087284713768672Shoga yangu, bila shaka kila mmoja wenu anajiandaa kupiga kura Jumapili ijayo kwa lengo la kumchagua kiongozi aliyemkuna kwa sera zake nzuri wakati wa kampeni.

Kikubwa ambacho nakuasa ni kuwa makini katika siku chache zilizobakia kabla ya zoezi hilo asije akatokea mtu na kukudanganya kwa fedha umpe kadi yako ya kupigia kura, utakuwa umefanya kosa kubwa!

Baada ya kukumbusha ishu hiyo muhimu, sasa narejea kwenye mada niliyokuandalia yenye kichwa hicho hapo juu, ni kweli kabisa shoga yangu kama umejaaliwa na Mwenyezi Mungu kuwa na shepu nzuri basi itumie kumridhisha mumeo.

Nasema hivyo kwa sababu kuna baadhi ya wenzetu pamoja na kujaliwa shepu f’lani hivi, wanashindwa kuwaridhisha waume zao kuanzia mavazi, mapishi, kuzungumza nao na hata kwenye yale mambo yetu.

Utakuta mwanamke kila anakopita wanaume wanamkodolea macho pima kwa jinsi mtoto wa kike alivyoumbwa akaumbika lakini ukimleta kwa mumewe anapata ziro kwa kushindwa kumridhisha.

Shoga yangu, ninapozungumzia kuhusu shepu yako simaanishi eti uwe na wowowo kubwa, macho makubwa, miguu ya bia, sauti nyororo la asha, hiyo uliyojaliwa na Mungu iliyomvutia mumeo mpaka akaamua kukuchukua jumla.

Nasema hivyo kwa sababu kila shetani na mbuyu wake, kama wewe ni mwembamba, mnene, una kifua kipana ukijumlisha na tabia yako nzuri ndivyo vilivyomvutia mumeo akaamua kukuoa.

Sasa kwa kutumia shepu yako mridhishe mumeo mnapokuwa katika eneo lenu la kujidai kwa kumfanyia kila utundu ili kumfanya muda wote akuwaze wewe na si wanawake wa nje.

Shoga, kumbuka kwamba bila ya wewe kujituma kwa kila nyanja pamoja na mambo ya chumbani zaidi, atashawishika kuchepuka jambo ambalo sipendi likutokee kwa sababu linaumiza na kuwatesa watoto hasa wazazi wanapoingia kwenye migogoro.

Hebu shoga yangu, itumie shepu yako vizuri kumridhisha mumeo, akikwambia kushoto geuka geuka, akikwambia angalia juu, fanya hivyo, akikutaka upinde mgongo upinde wala usimwambia unaumia au hutaki.

Kutotoa ushirikiano kwa mumeo wakati wa chakula cha usiku na mambo mengi kutamkwaza na kukuona hapati kile kitu roho inapenda na kuamua kuwasaka watakaomridhisha na wewe kubaki ukiwalea wanao huku yeye akiwa kahamia nyumba ndogo. Bye!


Loading...

Toa comment