The House of Favourite Newspapers

Shoga; Ukipendwa Hupendeki, Usipopendwa Je?

0

MFYUUUUU! Kwa hasira zangu nilizonazo nimeona ni heri nianze na kusonya kwanza ili angalau nipunguze jazba kidogo.

Haiwezekani mwanamke umempata mwanaume anayekupenda na kukujali halafu bado wewe unakuwa hujitambui, kila kukicha kiguu na njia.

Jamani! Mwanamke mwenzangu heshima ni kitu muhimu sana kwenye uhusiano wako.

Baadhi ya wapenzi wanashangaza sana, maskini unakuta mwanamme kajitolea kukupenda kwa kila namna lakini mwenzangu na mimi sasa, wala hupendeki, wala hujali! Unachukulia ize tu!

 

Shoga umeishajiuliza itakuwaje kama kuna siku ukiamka na kugundua mwenza wako hana mapenzi tena na wewe?

Shoga, mwenzako kajitolea kukupenda kwa moyo mmoja lakini kila anachojaribu kukufanyia unakuwa hupendeki, ueleweki hivi usipopendwa je, itakuaje?

Wakati mwingine nimekuwa nikijiuliza hivi mapenzi ni kitu gani hasa, mtu asipopendwa analalamika akipendwa nako bado analalamika. Nini tafsiri ya mapenzi! Utasikia akipendwa analalamika asipopendwa nako analalama! Hivi unataka ufanyiwe nini na mpenzi wako ndiyo ujue anakupenda, akununulie ndege wakati hana uwezo huo, akununulie bahari wakati hata kuogelea hajui!

 

Mwanamke mwenzangu, mtoto wa Bi Asha hebu kuwa na huruma na mtoto wa mwanamke mwenzako, mbaba wa watu anajitoa usiku na mchana kuhakikisha unapendeza lakini bado humthamini.

 

Kwa mfano kama mwanaume kampenda zaidi mwanamke, ni jambo la kawaida kusikia maneno ya kejeli kuwa “Shoga‘angu yule mwanaume kwangu hasikii wala aambiliki kwa chochote kile.”

 

“Kila ninapopita ananiganda kama ruba, nikigeuka hivi ana mimi, nikifanya vile ana mimi.”

Mwanamke mwenzangu

unapompata mwanaume wa kukupenda na kukujali jitahidi na wewe kung’ang’ania, wanaume wenyewe wakuoa, wako wapi shoga yangu siku hizi?

Eeeh! Jitahidi kumuonesha kuwa na wewe unatambua thamani na upendo wake kwake.

Mwanamke mwenzangu napata wakati mgumu sana ninapoona mwanamke mwenzangu unapata kila aina ya matunzo kutoka kwa mwenza wako lakini bado hutulii, bado ueleweki, hivi unataka nini? Unamtaka mwanaume wa aina ipi sasa katika maisha yako?

Kama mwanaume mpole, mwenye busara, mchapakazi, anayekujali, anakupenda na kukuheshimu wewe umepata, ndo kusema hulijui wala kuliona hilo? Shoga kama hujarogwa basi utakuwa na laana ya baba na mama kwa tabia zako.

Ukimpata anayekupenda pendeka shoga’angu kwani kutangatanga kwako unaweza kujikuta unaangukia kwa mtu ambaye hana mapenzi yoyote kwako zaidi ya kukuliza na kukuumiza kila kukicha.

Kama ni raha na utamu, mbona mapenzi ya kweli unapewa shosti wangu?

Kama ni raha mbona mpenzi wako anakupa lakini inafika sehemu shoga yangu uliyependwa unaona kama ni kero tena, unasahau kuwa ulikosa penzi la kweli la dhati.

Kama unapendwa hadi unaona kero, kwa nini umekuwa unanung’unika kuwa hupendwi kama unavyotaka, mfano umekuwa ukitamani kuwa karibu na mpenzi wako muda mwingi, tena muda wote akikuangalia na kukushika kimahaba, umesahau tena faraja uliyoihitaji na kuiona kero.

Usipopendwa tena unaona kama anayekupenda hakujali, ukipendwa pendeka acha kujishebedua kumbuka kuwa sehemu kubwa ya maisha yako imekuwa kwenye upweke uliokithiri, haujaliwi, haupendwi upoupo tu, huna thamani dhidi ya penzi lako, unahisi kama umeolewa au umeletwa kwa bahati mbaya.

Shoga’angu jifunze kumpenda anayekupenda kwa moyo wa dhati kuliko kuhangaika na mtu ambaye wala hakuwazii katika maisha yake.

Mwanamke mwenzangu jichunguze kwa makini zaidi,

Leave A Reply