The House of Favourite Newspapers

SHOGA; Ukitaka Kumuudhi Mbu, Lala na Neti!

HALOOOO ehhhh tena ya kisoda kama siyo bia, nitue Tanga kama siyo Muheza mwanakwetu wee wa Kibororoni utanieleza nini kama siyo kuishia Marangu Mtoni! Heee heeeiyaaaaa! Waambie na wenzako sasa Shangingi limepenya mwaka mpya! Na kwa taarifa yako tutabanana hapahapa mwaka huu! Ukipanda mnazi siye twapanda mchichaaaaa! Upo somo?

Shoga ulishaona wapi mtu analia huku anajifuta kwa kutumia shuka! Unaambiwa chozi la msibani halifutwi na leso! Halooooo eeeee! Inawezekana ati nimeanza kwa kasi ya ajabu kitu ambacho si kawaida yangu lakini kwa hilo sihitaji kukujulia hali kwa vile mwenyewe hutaki kuijua hali yako.

 

Najua kabisa ukisoma kichwa cha mada hii utaanza kujiuliza maswali mengi, mara ‘ohh Anti Naa mbona hatumuelewi, hiyo neti netiweki au anamaanisha nini? Weee nawee kama umetoka Mbarali huko Mbeya, kila kitu ushamba umekujaa hausigeli anayeshika rimoti ya TV akidhani ni simu.

Basi leo acha nikung’ate sikio shoga yangu wa ukweee mana mi na we tena! Shoga najua inafika kipindi lazima tuambiane ukweli kwa kweli maana kama kuruka siye wanawake tumezidi, tena wengine tunashindwa kutosheka kabisaaa sijui mwalimu wetu amekufaaa!

 

Nikisema hivi namaanisha ati! Juzi kuna shoga yangu alinifuata na kuniambia kuwa alilipata danga haswaaa, pande ya jamaa kama bodigadi wa wabeba vyuma au wale wa michezo ya mieleka! Mwili jumba kama siyo ghorofa! Basi hao wakaenda nyumba ya wageni, bahati mbaya wakati patashika kile walichokuwa wakikitumia kikapasuka, looo! Kuangalia huku na kule hawana tena nyingine!

 

Wote waliona uvivu kufuata kwa mhudumu mapokezi kwa vile kila mmoja alimuamini mwenzake hawezi kuwa na ugonjwa wa maambukizi. Kilichonishtua ni pale baada ya kwenda kavu danga likatangaza kuongeza dau mara mbili ya mwanzo. Kwa kuwa shostisto akili yake ilikuwa pesa tu, akakubaliana naye tena akajiachia kama yupo fukwe za huko Dubai!

Nilimuuliza hali ile imemtokea mara ngapi? Alisema siku ile ndiyo mara ya kwanza. Moyoni nilijua ni muongo, kwa vile tayari alikuwa amefanya kosa niliona ndiyo nafasi sahihi ya kuwaeleza mashostito wote wanaokimbilia madanga kisa pesa kujali afya zao kwani hakuna mtu wa kuzijali zaidi yao wenyewe.

 

Sikatai shoga, kuwa na madanga wakati mwingine ni kama biashara kubwa kwani wapo wanaotembelea magari na wengine wanamiliki miradi na majumba ya kifahari. Lakini la muhimu kuliko yote ni kuzijali afya zenu mnapokuwa hukooo! Hata mtu akiwa na umbile gani huwezi kumpima kwa macho, kama umekula vyake na anahitaji bidhaa yako basi hakikisha mnatumia kinga.

Jamani kwenye paketi zinakaa tatu, ya kwanza hajatosheka ya pili hajatosheka ya tatu bado? Aah! Jamani huo sasa ulafi nani alikuambia sigara ya kuokota inamaliza hamu.

 

Nanyi wanaume kwa nini jamani kwani nyama kwa nyama ndiyo mapenzi kwa kinga hainogi. Inawezekana kweli afya yako ni salama je, ya mwenzako?

Nawe shoga usikubali tena narudia usikubali kwenda kavu na mtu usiyemjua afya yake hata kama ana pesa vipi. Wengi waliokuwa wakidanga tumewazika au wengine wagonjwa. Siwahukumu walioambukizwa kwani naamini ule ni ugonjwa kama mwingine lakini tatizo lake mpaka sasa hauna dawa.

 

Ndiyo maana nakwambia hivi ukitaka kumuuzi mbu basi lala na neti au chandarua kama Waswahili wasemavyo! Sasa huyo mbu ukiona hataki utumie neti achana naye!

Kwa leo nipige breki hapa shoga!

Ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.

Comments are closed.