The House of Favourite Newspapers

Shoga; ukizembea rafiki yako atakupora mume!

0

Leo shoga yangu nitazungumza nawe mada yenye kichwa hicho hapo juu kufuatia baadhi ya wenzetu waliokuwa kwenye ndoa kujikuta wameporwa waume na marafiki zao wa karibu kisha kubaki wakilia vilio vya mbwa mwizi.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayependa kumpoteza mume au mke aliyetokanaye mbali, kumpoteza ninakokusema siyo kufa jambo ambalo haliwezi kuepukika katika maisha bali kuporwa na mtu mwingine.

Nasema hivyo kwa sababu tumeshuhudia jinsi watu wanavyokuwa na hasira inapotokea wamebaini wenza wao wanachepuka nje ya ndoa, hapo namaanisha wanawake kwa wanaume ambapo hutokea ugomvi unaosababisha majeraha au vifo.

Hata hivyo, wapo baadhi ya wanandoa wamejikuta wakiwapoteza wenza wao ambao huoa au kuolewa na watu wengine kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao. Hao sina neno nao isipokuwa wanawake wazembe.

Uzembe ninaouzungumzia; mfano kwa mwanamke aliyeolewa kuwaambia shoga zake namna anavyoridhishwa kimahaba na mumewe, utajiri wa mumewe na sifa zingine kibao ambazo zitasababisha marafiki zake kuanza kumzengea.

Shoga, hivyo ndivyo inavyotokea kwa wanawake wa mjini kwani nao watapenda kula sahani moja na mwanamke mpenda sifa anayetoa nje siri za mumewe na kama unavyofahamu mapenzi ni sanaa ikitokea mumeo kabaini huiwezi sanaa hiyo atapiga kambi la kudumu kwa shoga yako.

Awali wataanza kwa kujificha lakini kadiri siku zitakavyosonga mbele ni wazi wataweka wazi uhusiano wao kisha mumeo kukuacha bila kujali umezaa naye watoto na kumuoa aliyekuwa shoga wako wa karibu.

Hapo shoga yangu hautakuwa na mtu wa kumlaumu zaidi ya kujilaumu mwenyewe kwa kutoa nafasi hiyo kwa rafiki yako ambaye hukuwa na kiasi cha kumwambia mambo unayoyafanya na mumeo hususan umahiri wake kunako dimba la sita kwa sita nk.

Shoga, kuwa makini na marafiki zako na usitoe nafasi ya mumeo kuwa nao karibu kwani katika hali ya kawaida mwanamke na mwanaume hasa wasio ndugu wa damu wanapojenga mazoea ya kuwa karibu kitakachokea ni kuanzisha uhusiano wa mapenzi. Bye!

Leave A Reply