The House of Favourite Newspapers

Shoga; usafi huu kwa mumeo unakuhusu!

LOVE1Shoga, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu ni matumaini yangu kwamba afya yako ni njema na unaendelea na mapambano ya maisha.

Kwa upande wangu, familia yote tupo wazima na ‘Mkuu wa Kaya’ hajambo kishaenda kutafuta mkate wetu wa kila siku.Leo shoga yangu nataka kuzungumza na wewe kuhusu suala la usafi kwa ujumla ikiwa na ule unaopaswa kumfanyia mumeo tu!

Najua utakuwa unajiuliza ni usafi gani huo unaomhusu mumeo tu wakati kila kukicha unafagia ndani, kufua, kuosha vyombo na kuweka mazingira ya nyumba katika hali ya usafi nk.

Shoga, kuhusiana kuweka safi mazingira, kufua na mambo mengine ni wajibu wa mwanamke yeyote kwani asipofanya hivyo atachekwa kwa tabia ya uchafu.
Hata hivyo, usafi ninaotaka kuuzungumzia ni ule unaomhusu mumeo wenye lengo la kumfanya awe karibu na wewe muda wote.

Usafi huo unaanzia kwenye nguo zake zote yaani za nje hadi za ndani, kumkata kucha, usafi wa mwili na kumnyoa nywele zote.

Nafikiri ninapozungumzia nywele zote utakuwa umenielewe na kama hujaelewa basi utakuwa mtu usiyejiongeza unayependa kuambiwa moja kwa moja bila kutumia tafsida, hivyo utanisamehe.

Shoga yangu, hakuna kitu wanachokipenda wanaume wengi kama kufanyiwa usafi na wake zao hususan kusuguliwa maeneo mbalimbali wakati wa kuoga.
Kukakatwa kucha na wake zao hasa siku za wikiendi wanapokuwa wamepumzika nyumbani, kunyolewa bustani zao na nywele za kwapani.

Ukiona unamfanyia usafi huo mumeo halafu hatulii nyumbani ujue huyo hajatulia lakini kwa walio wengi wanapofanyiwa hivyo na wake zao siku za wikiendi hawatoki nyumbani na wakitoka watakuwa na wake zao.

Comments are closed.