The House of Favourite Newspapers

Shoga; usichepuke kisa, mumeo ‘njaa kali’

0

Vanessa3Kabla sijaanza kuzungumza nawe kuhusu nilichokuandalia, sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye anazidi kuniongezea dakika za kuvuta pumzi.
Baada ya kusema hayo sasa narejea kwenye mada niliyokuandalia ambayo imebebwa na kichwa hicho hapo juu.

Shoga yangu, huo ndiyo ukweli kwamba usichepuke nje ya ndoa kwa sababu kipato cha mumeo ni kidogo a.k.a ‘njaa kali.’

Hakuna kitu kibaya katika maisha ya ndoa kama mwanamke kumsaliti mumewe kwa vile uwezo wake kiuchumi siyo mzuri.

Mwanamke anayefanya hivyo moja kwa moja inaonesha aliingia kwenye ndoa kwa malengo f’lani na siyo mapenzi ya dhati kwa sababu kama alimpenda mumewe toka moyoni ni wazi angedumisha upendo na mambo mengine ni matokeo.

Nasema ni matokeo kwa sababu anayetoa riziki ni Mwenyezi Mungu tena huitoa kwa wakati wake, mume leo anaweza kuwa hoehae wa kutupwa lakini kesho akawa bilionea.

Shoga yangu, kumbuka kwamba kuna baadhi ya wanawake leo wanajuta baada ya kuwakimbia waume zao kisa hawakuwa na fedha na baada ya kufanya hivyo huku nyuma Mungu akafungua milango ya baraka kwa waume zao na kuwa wenye fedha na mafanikio makubwa.

Mbaya zaidi wapo wenzetu kwa vile waume zao ni njaa kali huwapa masharti hata ya kula chakula cha usiku.Siku jamaa wakiwa na senti au wameleta chakula kizuri ama kuwanunulia nguo na zawadi zingine ndizo wanazowapa haki yao ya ndoa.

Kufanya hivyo shoga yangu ni kuwanyanyasa waume zenu na hata Mungu hapendi, hivyo ishini kwa mapenzi ya dhati kwa sababu asiyekuwanacho leo huenda akawanacho kesho.

Leave A Reply