Shoga; usimkomoe mumeo kwa kero za kazini kwako!

neyoShoga yangu, kwa kuwa siku za kupiga kura kumchagua rais, wabunge na madiwani zimekaribia naendelea kutoa rai kwa kila mmoja kuhudhuria kwenye mikutano ya kampeni kusikiliza sera za wagombea ili Oktoba 25 ikifika muwachague viongozi bora.

Leo shoga yangu nataka kuwazungumzia baadhi ya wenzetu wanaofanya mambo ndivyo sivyo kwa waume zao na kusababisha mifarakano ndani ya ndoa.

Kawaida katika harakati za kutafuta riziki ambazo zimegawanyika kwa baadhi ya watu kufanya shughuli za ujasiriamali na wengine kuajiriwa kuna changamoto zake.

Miongoni mwa changamoto hizo, kwa walioajiriwa kufokewa na viongozi wao wa kazi kufuati kuchelewa kazini au kuharibu kazi nk.

Kwa waliojiajiri mfano wafanyabiashara, biashara kutokwenda vizuri au kupata hasara au kukorofishana na wengine nk.

Mambo hayo yanapomkumba mtu yeyote, humharibia mudi yake ambapo kwa mtu asiye makini hasira za kufokewa na bosi au kucheleweshewa mshahara atazipeleka nyumbani.

Hali hiyo inaweza kumkumba baba au mama lakini walengwa wangu ni wanawake kwa sababu safu hii ni mahususi kwao. Kuna baadhi ya wanawake wakikutana na masaibu hayo, waume zao wanapohitaji chakula cha usiku huwawekea ngumu.

Shoga yangu, kufanya hivyo ni kosa kubwa sana na ukisikia watu wanasema mwanamke mjinga huibomoa nyumba yake kwa mikono yake ndiyo huwa hivyo.

Hivi kweli shoga yangu kero za kazini kwako unazitumia kumkomoa mumeo kumnyima haki yake iliyokufanya uungane naye na kuwa mwili mmoja?

Kufanya hivyo ni kosa kubwa, ikitokea umekasirishwa na jambo f’lani unapokutana na mumeo sahau kila kitu ili umfurahishe kwa mapishi, usafi wa nyumba na mwisho akihitaji kuwa na wewe kunako sita kwa sita mpe chakula chake ale afurahi naye atakufurahisha pia.


Loading...

Toa comment