The House of Favourite Newspapers

Shoga; usipoji-shusha kwa mumeo utaachwa!

0

Vanessa3Shoga, ni matumaini yangu ulisherehekea vizuri Sikukuu ya Pasaka na familia yako akiwemo mkuu wa kaya.

Kwa upande wangu namshukuru Mungu ilikuwa nzuri sana kwani mwaka huu nilikwenda Mbuga ya Mikumi na shemeji yenu kubadilisha upepo kidogo.
Leo shoga yangu nataka kuzungumza nawe kuhusu tabia waliyonayo baadhi ya wenzetu kutopenda kujishusha mbele ya waume zao badala yake huwapanda vichwani.

Shoga, hakuna kitu kibaya kwa mwanamke kama kujiinua kwa mumewe na kufikia hatua ya kumkaripia kama mtoto mdogo.
Huwa najiuliza na kushindwa kupata jibu inakuwaje mpaka mwanamke kufikia hatua mumewe anapomuonya au kumwelekeza jambo badala ya kuwa mpole anaanza kumjibu kwa jeuri na kumwambia kama amemchoka ampe talaka yake.

Kwa mwanamke aliyelelewa vizuri na kupata mafunzo kabla ya kuolewa kufanya hivyo ni aibu kwake na kwa wazazi wake.
Cha ajabu ni pale mama anapomjia juu mumewe anapohitaji kupata ‘chakula cha usiku’ kwa kumwambia;
“Bwana eh nimechoka kwani umesikia usipokula chakula cha usiku utakufa, kamtafute huyo anayeweza kufanya hivyo kila siku!”
Shoga, unafikiri utakapomwambia hivyo mumeo kitafuata nini kama siyo kumtafuta mwanamke wa nje ili afurahie maisha?
Kikubwa shoga yangu ni kujishusha kwa mumeo na kuacha kutumia lugha isiyofaa kinyume chake utaachwa wakati bado unampenda mista wako. Bye!

Leave A Reply