The House of Favourite Newspapers

SHOGA; Uwanja Hauhitaji Aibu

0

 

Haya haya tena shoga yangu wa ukwee!  Kama kawa nimerudi tena kama moto wa tipa usiozimwa na magari ya zimamoto yenye tenki la ujazo la maji ya kuoga pengine utoke bafuni na sabuni mwilini ama povu, aku babu lazima nikwambie ukweli maana moto wangu lazima bahari ikauke ndipo ufanikiwe kuuzima, upo?

Haya tuendelee na yetu hasa yaliyonifanya nifungue mdomo wangu MC Sophy miye! Kuna baadhi ya wanawake wananiudhi sana kufikia hatua ya kukosa raha, unamuonea haya mumeo au mpenzio mkiwa ndani full khanga sipendi eeeh! Umesikia mwili wako mkiwa faragha si mali yako bali ya mwenzako.

Unauficha una kasoro gani mwenzio anahitaji kuliona umbile lililomvutia likiwa na nguo ameliweka ndani ili alifaidi kwa kuliona live, wewe na mikhanga kutwa kucha hata kujipaka mafuta ya mgando hujipaki mbele ya mwenzio heee heeeeiyaaaa!

Mumeo amekuwa akihangaika kuutazama mwili wako kama wewe siyo wake, hupendi kula naye chakula hata cha mchana na usiku unazima taa! Wee nawe vepe umerogwa?  Kufanya hivyo ni kumnyima haki ya msingi mpenzi wako.

Hauko pale kwa ajili ya kuvua nguo za ndani tu, la hasha mwanamke ni pambo la nyumba unatakiwa ujiachie muda ukifika bibi wee! Hasa ukijua mwenzio anarudi toka kazini kujiweka kwako kwa kuvaa upande mwepesi wa khanga tabasamu halitoki mdomoni, mashamsham ya kumwaga, upo?

Shoga kuna jamaa mmoja alioa binti aliyeumbwa akaumbika lakini binti yule alikuwa anamuogopa mumewe kwa kuona kukaa bila nguo mbele ya mumewe kwake ilikuwa aibu kubwa! Muda wote alikuwa na khanga hakupenda kula chakula mchana, alipolazimishwa sana alikuwa akifunga madirisha na kuvulia nguo kitandani na mumewe akimaliza alikuwa anawahi kuvaa khanga.

 

 

Mtindo ule ulimsumbua sana bwana huyo aliyekuwa na hamu ya kuuona mwili wa mkewe ambao Mungu aliamua kufanya utundu wake ukimuangalia utafikiri kauchora na kupendelewa na mchoraji.

 

Mzee mzima uzalendo ukamshinda na kuamua kutafuta njia ya kuuona mwili wa mkewe bila yeye kujua. Alianzisha mtindo wa kumvizia wakati wa kuoga kumpiga chabo, kutokana na kupata shida ya kuufaidi mwili wa mkewe jamaa aliamua bora awe anapanda juu ya mti ili aweze kumuona vizuri, hilo nalo neno ati!

 

Jamaa alifanikiwa kupanda juu ya mtu na kumtazama vyema mkewe aliyekuwa akioga, hakuamini chakula kitamu kama kile kukilia gizani. Kutokana na kiwewe alijisahau kushikilia mti na kuporomoka toka juu ya mti mpaka chini, loo!

 

Jitu zima acha watu wamshangae kwa kumpiga chabo mkewe mtu anayelala naye kitanda kimoja, shuka moja, miguu na kifua vimekumbatiana. Jamaa alijitetea kwa kusema ukweli kuwa amekuwa akipata shida kuuona mwili wa mpenzi wake.

 

Ilibidi yule mwanamke awekwe chini na kuelezwa ukweli juu ya tabia yake inayoweza kumpeleka kubaya mumewe.

 

Baada ya yule mwanamke kugundua kosa lake alipojiachia mumewe alichanganyikiwa, kila baada ya kazi aliwahi kurudi nyumbani, Jamani kujiachia kwa sehemu maalum kwa mwandani wako ni tiba ya kumfanya atulie nyumbani. Hata kama unajisikia basi jipitishe mbele na upande wa khanga halafu jifanye umekudondoka kwa bahati mbaya, kabla ya kuidondosha kohoa kidogo lazima ataangalia hapo idondoshe.

 

Usimuangalie jifanye humuoni lazima atakuwa anakuangalia akifahamu humuoni, iokote taratibu huku ukimuachia aisome namba. Nakuapia lazima mzuka utampanda na kutamani kitu. Usimnyime ni haki yake kukupa raha.

 

Usimtese mwenzio muoneshe kilichomfanya akuchague na kukuficha ndani.
Kwa haya machache tutapunguza kuzurura kwa waume zetu baada ya kazi.

Tukutane tena wiki ijayo!

Leave A Reply