The House of Favourite Newspapers

Shoga; wape na wenzio maujuzi

0

Asalam alaikum wapenzi wasomaji wangu, leo nimekuja kuwakumbusha makungwi wenzangu kuacha uchoyo.

Si unajua tena mimi nimestaafu, sasa nikikaa pembeni na kuona mashosti hawana ujuzi wakati walio karibu yao ni mahodari ndiyo nashangaa iweje una mautundu unashindwa kuwapa na wenzako ili wafuzu kwenye ndoa zao?

Shoga kumbuka shosti yako ni ndugu yako, hivi kwa nini usimfanye ndugu yako akawa na heshima kama uliyonayo wewe huko faragha.

Kuna shosti mmoja alinifuata na kuniambia kuwa hajui jinsi ya kuzungusha nyonga awapo faragha na mumewe hupendelea kitu hicho, nilimshangaa moyoni, lakini nikamwambia nitamfundisha na ataiva, naye alinishangaa kwani alisema alishamaliza pesa zake kwa makungwi na mashosti zake ili tu wampatie ujuzi.

Hivi shosti unadhani kumfundisha mwenzako mautundu ya chumbani ndiyo atakuchukulia mume? laa, jinsi unavyomfundisha ndiyo ujuzi wako unapozidi kukua siku hadi siku.

Sasa basi kwa nyie ambao hampendi kutoa ujuzi, niwafahamishe tu hata nyie bado mnahitaji ujuzi wa chumbani kwani maisha ya mapenzi kila siku yanabadilika, unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unatoa ujuzi kwa wenzako na wewe unasaka kwa wengine, usipotoa ushirikiano unadhani utapewa?

Jinsi ya kuwafundisha

Kaa na shosti wako, mchunguze kwa umakini kinachomsumbua, baada ya hapo muweke tayari ili akubaliane na mafunzo yako kwani si kila mwanamke yuko tayari kuweka wazi upungufu wake kwa mumewe.

Wengine wanahisi kuweka kwake wazi unaweza kuutumia udhaifu huo kumchukulia, akishaweka wazi sasa funguka na umfundishe.

Wanawake wengi wanajua kumpikia mume, kumpa faragha ndiyo kila kitu ila kuna utundu unaohitajika chumbani ambao wengi hawaujui, sasa utundu ulionao wewe mpe na mwenzako.

Mfano, mfundishe jinsi ya kumpokea mume akiwa na hasira, jinsi ya kumtuliza na kumuingiza kwenye faragha na kila mtu akaridhika, mfundishe jinsi ya kumfanya mume aliyechoshwa na ‘stress’ kuwa mwenye kufurahia ndoa, wanawake wengi hawayajui haya.

Shosti, mume anatakiwa kuchukuliwa kama mtoto anayenda kubembelezwa muda wote na si vinginevyo.

Bila shaka mmenielewa, kwa mwenye shida anaweza kuniandikia ujumbe mfupi kupitia namba hii  0788224474 ili nifundishe kwa niaba ya wote wenye matatizo yanayofanana na hilo.

Leave A Reply