Shoga;Mumeo Umepewa Na Mungu Jiachie Utakavyo!

Shoga, ni matumanini yangu kwamba upo mzima na unaendelea na maisha baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao ulikuwa na changamoto nyingi na kutuweka mioyo juu kwa presha ya kupanda na kushuka.

Kikubwa shoga ni kumaliza tofauti zetu za kisiasa kwa sababu Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( Nec) imemtangaza Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Nne wa taifa letu.

Baada ya kusema hayo ngoja nirejee kwenye jambo ambalo nimekuandalia linalokutaka kuwa mpya kila siku katika ndoa yako ili kumdhibiti mumeo atulie nyumbani kwa sababu ukizembea tu wenzio watambeba jumla.
Shoga yangu, katika maisha hakuna mtu ambaye hapendi kuwa na kitu kipya, jambo hilo halipo na kama yupo basi mtu huyo atakuwa na tatizo f’lani.

Nasema hivyo kwa sababu hata nguo zetu zinapopauka au kuchakaa huwa tunaacha kuzivaa na kununua mpya lengo likiwa ni tupendeze.Linapokuja suala la mapenzi, kila mtu hupenda mwenza wake awe mpya asiyechosha wanapokuwa kwenye uwanja wa fundi seremala.

Upya ninaouzungumzia ni mwanamke aliyeolewa kujiongeza katika kila idara kuhakikisha muda wote mumewe anamuwaza na kumdhibiti asiwawaze michepuko.Mwanamke lazima uwe mbunifu wa mambo ya chumbani zaidi kadiri siku zinavyokwenda mbele, jua namna ya kumdekea mumeo, kumbembeleza na kumhamasisha kimalovee ili kila wakati awe na hamu ya kuwa nawe.

Mhamasishe mumeo kwa kumvalia nguo za mitego muwapo wawili chumbani au nyumbani kwani akiiona shepu yako ‘tamu’ ni wazi atakupa raha mtoto wa kike.

Huo ndiyo upya ninaouzungumzia badala ya kuvaa nguo ndefu zilizokuziba mwili wote vaa nguo nyepesi ambazo zitaonesha kila kitu kilichomo mwilini mwako kwani mumeo umepewa na Mungu jiachie utakavyo mwana kwetu ili afurahi. kisha akufurahishe pia. Bye!

Loading...

Toa comment