Sholo, Man Fongo Kumaliza Ubishi Dar Live

Sholo Mwamba

WAKATI siku zikielekea kukatika kufikia Aprili Mosi (Sikukuu ya Pasaka), Staa wa Singeli, Sholo Mwamba kwa mara ya kwanza anatarajia kukutana uso kwa uso na wakali wenzake wa muziki huo, Man Fongo na Dulla Makabila ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Mratibu na Meneja wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ aliiambia Risasi Vibes kuwa usiku huo wakali wao wa Singeli watatambiana na kujua nani mkali kwa mwenzake.

Man Fongo

 

“Pata picha wakiwepo jukwaa moja Makabila, Man Fongo na Sholo Mwamba panakuwaje? Niwaombe tu mashabiki hii si ya kukosa kwani kutakuwa na amshaamsha mwanzo mwisho mpaka kielekewe,” alisema KP na kuongeza;

“Mbali na wakali hao wa Singeli, jukwaa pia litawapambanisha makundi yanayotamba kwenye Taarab, Yah TMK pamoja na Jahazi Modern ambapo napo mpaka kieleweke nani anaweza fujo za mjini huku burudani zote hizo ukizipata kwa mtonyo wa buku 7 tu getini yaani 7,000.”

Katika usiku huo pia kutakuwa na michezo kibao kwa watoto itakayoanza kuanzia saa mbili za asubuhi kama vile kuogelea, sarakasi, kuteleza, kubembea na mingine mingi kwa kiingilio cha shilingi 3000 tu getini.
Toa comment