The House of Favourite Newspapers

Sholo,Man Fongo watunishiana misuli Dar Live

Man Fongo.

 

ILIKUWA ni Pasaka ya aina yake ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar ambapo Jumapili iliyopita ilifanyika shoo kubwa ya aina yake huku wakali wa Singeli, Sholo Mwamba na Man Fongo wakitunishiana misuli.

 

Shoo hiyo iliyotambulika kama Mwisho wa Ubishi, ilianza kwa burudani ya Muziki wa Mwambao kutoka kwa makundi tishio ya Yah TMK Modern pamoja na Jahazi Modern chini ya Prince Amigo.Shoo ya kibabe ilianza mida ya saa sita kwa wakali wa Singeli ambapo mkali Dulla Makabila aliingia na kuwapagawisha mashabiki kwa nyimbo zake zote kali kuanzia Makabila hadi Haujaulamba.

 

Sholo Mwamba aliingia kwa mbwembwe akiwa na madansa wake waliovalia nguo za njano zinazofanana na sare za wafungwa wa magereza ambaye naye aliamsha mwanzo mwisho na ngoma zake hatari zikiwemo Ghetto, Kama Ronaldo na Sembe Tembele.

Sholo Mwamba

 

“Sholo Mwamba si wa nchi hii, bonge la shoo na nimeinjoi kwa kweli,” alisema shabiki mmoja wa Singeli. Naye Man Fongo aliwapagawisha na ngoma zake za Nani Asiyependa, Safi Tu pamoja na Hainaga Ushemeji ambapo alikuwa akiimba na kucheza na mashabiki mwanzo mwisho.

 

Wakizungumzia shoo hiyo mara baada ya kushuka stejini, wakali hao wa Singeli kila mmoja alionesha tambo.“Nadhani mashabiki wenyewe wamejionea nani mkali, shoo ilikuwa safi na nimefanya kile kinachotakiwa,” alisema Man Fongo.

 

“Tatizo time na yenyewe inabana, nilikuwa tayari tuendelee kupambana mpaka majogoo, kutoboa ilikuwa inawezekana lakini freshi tu mashabiki wote wamejionea shoo nzima na majibu wanayo kichwani mwao,” alisema Sholo Mwamba.

Risasi Vibes.

Comments are closed.