The House of Favourite Newspapers

Shoo ya Kibabe Yatikisa Dar Live Mkesha wa Mwaka Mpya 2018

Msanii Coyo akikamua.

WAKALI wa Bongo Fleva, Coyo, Q-Boy na wengine jana walifunika katika Show ya Kibabe iliyofanyika kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya 2018 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

Baada ya hapo Msanii Coyo alipanda na kuimba na mashabiki wake karibu kila nyimbo, Msanii Ice Boy naye alifanya vizuri sana.

Kwa upande wa msanii Q Boy Msafi, yeye alipanda jukwaani akiwa amevaa ova roli na usoni akiwa amejifunika kwa maski huku Jay Mo akiwaimbisha Wimbo wa Nisaidie Kushare mashabiki waliofurika uwanjani hapo.

Massai akifanya yake.

Mwingine aliyefanya vizuri ni Msanii Young Killer, Stamina ambao waliunyanyua umati wa mashabiki kwa shangwe waliofurika Dar Live na kuanza kuimba nao.

Show ya Usiku wa Kibabe ulipambwa na keki nzuri ambayo ilipandishwa jukwaani na mtangazaji maarufu Bongo, Maimatha wa Jesse ambapo mshabiki walipata nafasi ya kusherekea mwaka mpya kwa kula keki na kusindikizwa na shangwe za matarumbeta.

Host wa Show ya Mkesha wa Mwaka Mpya 2018 ulisimamiwa na mkali Shebby na mchekeshaji maarufu Bongo Dullvan.

 

 NA ISSA MNALLY | GPL

Comments are closed.