The House of Favourite Newspapers

Shoo ya Pacha Milionea, Davido Ilivyobuma

0

davido

MACHALII wenye asili ya Tandale, wanaopeperusha bendera ya Bongo kwa Trump (USA), Mapacha Milionea, wanadai kufanyiwa figisu kwenye shoo iliyokuwa wapafomu na mkali wa ngoma ya Blow Your Mind kutoka Nigeria, Davido.

 

Wakibonga na OVER ZE WEEKEND kutokea Boston, Marekani, Elisha na Elia Kimanga wamesema aliyevuruga mchongo huo ni promota ambaye walikuwa na makubaliano naye ya kuwaunganisha na Davido ambapo licha ya makubaliano kufanyika, siku ya shoo ilipofika, promota huyo aliwachenjia dakika za mwisho na kuwapandisha wasanii wengine tofauti.

 

“Ilituuma, ile ilikuwa ni platform nzuri sana kwetu ya kujitangaza Afrika nzima na duniani kote. Davido alikuja kufanya shoo Boston, tukayajenga naye, akakubali kila kitu, sema promota ndiyo akaja kuleta mizinguo,” alisema Elisha.

 

“Hata hivyo bado hatujakata tamaa, ngoja huu msala wa Corona uishe, tuna mipango kama yote, lazima tutoboe na dunia nzima itujue! Tayari tunafanya poa na ngoma kama Trumpet, Again, Zuzu, Paradise na Come On! Come On! Tunaomba Wabongo watuunge mkono, tunaipeperusha vizuri bendera ya Tanzania huku kwa Trump,” alihitimisha Elia.

STORI: OVER ZE WEEKEND

Leave A Reply