Shoo ya ‘Piga Nikupige’ Dar Live Yaacha Gumzo – Video

Issa Kamongo wa Zanzibar Stars akiwa jukwaani.

USIKU wa mpambano wa bendi tatu za taarabu na wasanii wa singeli uliokwenda kwa jina la Piga Nikupige uliofanyika jana (Jumatano) siku ya Idd Al Haj ulikuwa ni zaidi ya burudani kwa jinsi makundi hayo yalivyofunikana katika kuwanogesha mashabiki waliofurika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, Dar.

Mpiga gitaa wa Zanzibar Stars, Rajab Kondobesi,  akionyesha umahiri wake jukwaani.

 

Bendi zilizotifuana katika mpambano huo zilikuwa ni Hurricane, Jahazi na Zanzibar Stars Modern Taarabu ‘Wana Nakshinakshi’ ambapo baada ya mtifuano huo wasanii wa singeli nao walipewa nafasi ya kuonyesha umahiri wao.

Mwanamkuu Zayumba wa Zanzibar Stars akiimba jukwaani.

 

Burudani hizo ziliwafanya mashabiki waserebuke mwanzo-mwisho kufuatia kunogeshwa na burudani hiyo.

Zena Mohammed wa Zanzibar Stars akiwa kazini.

 

Mashabiki wakijimwaya.

Miriamu Amour wa Jahazi.

Fatma Kassim wa Jahazi ambaye ni mdogo wa mwimbaji mkongwe wa taarab Jokha Kassim. 

Mashabiki. 

Mwimbaji wa singeli, Pazo Mreno,  akichagiza mashabiki.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL


Loading...

Toa comment