The House of Favourite Newspapers

Shuhudia Video ya Majambazi 8 Walioteka Gari Walivyokamatwa

 

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani wamefanikiwa kukamata majambazi nane waliohusika na tukio la utekaji wa gari lenye namba za usajili T.311 DHS aina ya Fuso, tukio lililotokea eneo la Vigwaza Wilaya ya Kipolisi Chalinze lililokuwa likiendeshwa na Abeid Victor akitokea Jijini Dar Es Salaam kwenda Mkoani Iringa.

 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mkoani hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shanna amesema tukio hilo likitokea baada ya watu wawili waliojifanya wasamaria wema kumsimamisha dereva huyo wakihitaji msaada ndipo walipo mgeuka na kupora gari hilo lililokuwa limebeba unga wa ngano mifuko 250.

 

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na askari wa Mkoa wa Morogoro waliendesha msako mkali na kufanikiwa kuwakamata majambazi hao. Aidha majambazi hao wamehojiwa na kukiri kuhusika na tukio hilo kisha wakawapeleka askari katika eneo walupokuwa wamehifadhi mzigo huo na vifaa vya gari vilivyokuwa vimekatwa ambavyo ni kichwa cha gari hilo (Cabin), Kadi ya gari hilo lenye namba T.311.

 

Kamanda Shanna amewaasa wananchi kutoa ushirikiano na kuwafichua watu wasiowaelewa kwenye maeneo yao ili waweze kuwafuatilia kwa karibu na wale watakao bainika kuwa ni wahalifu waweze kuwakamata.

 

Katika tukio la pili mtu mmoja amepoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka jana majira ya saa 15:45 Alasiri katika kijiji cha Mwidu barabara ya Dar es salaam Morogoro, aliyefariki katika ajali hiyo ni dereva wa gari aina ya Benz yenye namba DHU yenye namba T.561 DHUaliyetambulika kwa jina la Michael Mndasha mwenye umri wa miaka 34 mkazi wa Tegeta Dar es Salaam na mtu mwingine ambaye amejeruhiwa ametambulika kwa jina la Gabriel Semiono mwenye umri wa miaka 26.

 

GOOD NEWS: Majambazi 8 Walioteka Gari Wamekamatwa

Comments are closed.