SHUKA LA KUAZIMA HALISTIRI BARIDI

PAMBEEEE heeeee unashangaa kumuona kuku kwa mganga umesahau kama rangi yake ndiyo imemroga! Wareeee reeee unachezea bomba wakati umevaa kijora! 

 

Shoga mjini wanakwambia usidharau mkaa kwa kupata jiko la gesi siku yoyote linakuzimikia unarudi kulekule, haloooo eeeehhh! Kama nakuona unavyohangaika kufuta picha Whatsapp umesahau kama kwenye Facebook zipo!

 

Napenda sana kuchangamka tena kila siku lakini lazima kuna kitu kitaingilia kati na kunikwaza. Baada ya kuwaon-gelea wana-wake wenza-ngu karibu mara tatu mful-ulizo shoga leo nipo na nyie kina baba ambao hamna mbele wala nyuma.

 

Nikisema huwa namaanisha ati! Juzi nimetumiwa meseji na rafiki wangu wa siku nyingi ambaye nimepotezana naye na kuniambia kuwa kwa sasa umri unakwenda na bado hajaolewa. Nilipomuuliza kwa nini ndiyo akaanza kutiririka sasa!

 

Anasema kuwa, baada ya kuzalishwa mtoto mmoja na mwanaume mwingine akaachika lakini kila anayempata anaishia kumchezea na likija suala la ndoa basi wanamkimbia na kwenda kuoa kwingine. Basi shoga yangu huyo akanipa na mifano ya marafiki zangu wengine ambao tulishawahi kuwa pamoja nao kisa wameachika wamekosa kabisa wa kuwaoa.

Nikugeukie sasa wewe baba ambaye ukishasikia mwanamke kaachika au ana mtoto basi unaona huyo si wa kumuoa! Unajua sababu ya kuachika kwake, unajua sababu ya kupata mtoto kabla ya kutaka kumuoa?

 

Natamani sana siku moja wanaume wote wawe wananisikiliza na kufanyia kazi ushauri wangu lakini hata kupitia hapa wapo watakaonielewa. Jamani kwa nyie wanaume mnaotaka kuoa ukishaingia kwenye uhusiano na mwanamke ukajua kuwa aliachika ni vema basi ukafuatilia kujua sababu iliyomfanya akaachika.

 

Wengine wameachika kutokana na tabia za mwanaume labda kupenda wanawake wengine wakati yupo kwenye ndoa au uhusiano. Wengine wameachika bila kuwa na sababu za msingi mwanaume kaamka tu kaamua kumuacha!

 

Ndiyo maana wakati mwingine nasema shuka la kuazima halistiri baridi, wanaume wengine nawaona kama shuka la kuazima kila mwanamke wao wanaona kama kipoozeo, shuuuutuuu! Shoga leo nisiongee sana maana limenikaa hapa! Tukutane tena wiki ijayo tu kwa mada nyingine. Ni mimi Anti Naa Shangingi Mstaaf.

Toa comment