The House of Favourite Newspapers
gunners X

Shule 10 Bora Kidato cha Nne 2020, Matokeo Haya Hapa!

0

 

BARAZA la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato nne mwaka 2020 na kuzitaja shule 10 zilizofanya vizuri huku Shule ya Wasichana ya St Francis ya mkoani Mbeya ikishika nafasi ya kwanza kitaifa.

 

St. Francis imepanda kutoka nafasi ya pili iliyoshika mwaka juzi na kuishusha Shule ya Sekondari ya Kemebos ya mkoani Kagera hadi nafasi ya nne.

 

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo (Januari 15, 2021), Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, amezitaja shule nyingine zilizofanya vizuri zaidi katika matokeo hayo kuwa ni Ilboru ya mkoani Arusha, Cannosa (Dar es Salaam), Kemebos (Kagera) na Feza Boys ya jijini Dar es Salaam.

 

Nyigine ni Ahmes, St Aloysius Girls, Marian Boys (Pwani) na St. Augustine Tagaste ya jijini Dar es Salaam. Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam imefanikiwa kuingiza shule tatu kila moja katika orodha hiyo ya dhahabu, huku Katika orodha hiyo, Serikali imefanikiwa kuingiza shule moja tu ya Ilboru huku zilizobaki zikiwa ni shule binafsi.

 

Kupata matokeo >>>>> Bofya Hapa

Leave A Reply