The House of Favourite Newspapers

Shule tano za mkoani Mwanza zafungwa baada ya Kipindupindu kuua wanane

0

mwanza_town

MLIPUKO wa ugonjwa wa kipindupindu umeshika kasi sasa mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Singida na Mwanza baada ya kusababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kulazwa mahospitalini tangu ugonjwa huo uanze kusambaa kwa kasi nchini mwanzoni mwa Agosti.

choleraBakteria aina ya vibrio chorelae ambao husababisha ugonjwa wa kipindupindu

Hali inazidi kuwa mbaya katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na mlipuko wa kipindupindu, hali iliyopelekea Shule nne za Msingi na moja ya Sekondari katika Kata ya Irugwa wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, kufungwa kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo kisiwani humo.

Shule za msingi zilizofungwa ni za Buruza, Nabweko, Sambi na Kulazu, wakati shule ya Sekondari ya Irugwa zote zimefungwa leo baada ya wanafunzi 22 wa shule za Msingi Nabweko kuambukizwa kipindupindu na watu wengine waliokuwa wanakusmbuliwa na ugonjwa huo kufariki dunia.

Diwani wa kata hiyo ya Irugwa, Juma Msongi ameithibitisha kuwa, tangu ugonjwa wa kipindupindu ulipoikumba kata yake wiki iliyopita katika baadhi ya maeneo ya Kata hiyo, watu 8 wamefariki dunia na hali inazidi kuwa mbaya kutokana na kukosekana kwa huduma madhubuti za kuweza kukabiliana na ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa diwani huyo, kutokana na hali ilivyo sasa wananchi wanatakiwa kuzingatia usafi wa mazingira ikiwemo matumizi sahihi ya vyoo na kujiepusha na ulaji ovyo wa vyakula, kuhakikisha usafi wa mazingira, vyakula na kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu.

Leave A Reply