The House of Favourite Newspapers

Shule ya Miti Iliyompa Wakati Mgumu Nape Nnauye – VIDEO

 

MBUNGE wa Jimbo la Mtama, Nape Nauye amefanya mabadiliko makubwa kwa muda wa miaka miwili na nusu katika jimbo lake la hilo akitekeleza ahadi alizowaahidi wananchi wake katika kuboresha sekta ya Afya, Elimu, Kilimo, Maji na Kuondoa Umaskini.

 

Shule ya Msingi Litingi ni miongoni mwa shule zilizozua gumzo hapa nchini kwa kushambuliwa kwa maneno na baadhi ya Watanzaniahuku wengi wao wakiumizwa na hali ya muonekano mbovu wa shule hiyo iliyokuwa na darasa moja tena likijengwa kwa miti na kuezekwa mabati na kutumikakwa wanafunzi wa darasa la kwana hadi la saba.

Wanafunzi walipata shida wakati wa kiangazi na wakati wa Mvua hali iliyopekea wanafunzi wengi kukosa motisha ya kusoma, lakini kupitia juhudi za Mbunge wao, Nape Nnauye amefanikiwa kuwajengea madarasa ya kisasa na kujenga nyumba ya mwalimu, kumwekea sola na sasa ujenzi unaendelea.

 

VIDEO: SHUHUDIA SHULE HIYO NA NAPE AKIFUNGUKA

Comments are closed.