The House of Favourite Newspapers

Shule ya Sekondari Chifunfu Yaongoza Matokeo ya Kidato cha Nne Sengerema

0

Shule ya Sekondari Chifunfu iliyopo Kata ya Chifunfu wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza imefanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2023.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Chifunfu, Dotto Ndemella amesema siri ya mafanikio ya kufanya vizuri katika matokeo hayo ushirikiano kati ya walimu, wanafunzi na wazazi ambao wamejitoa kuleta chakula kwa ajili ya watoto shuleni.

Sambamba na usimamizi wa elimu, uongozi bora, nidhamu kwa wote, kufanya mazoezi mengi ya mitihani kila mwezi na madarasa ya mitihani hufanya mazoezi kila wiki.
Ndemella amesema tangu achaguliwe kuongoza shule hiyo Machi 2023 akitokea Shule ya Sekondari Kilabela ambako alikuwa mwalimu wa taaluma alikuta shule hiyo haijafuta daraja sifuri huku ufaulu wao ukiwa daraja la nne na daraja la kwanza hadi la tatu ufaulu ulikuwa chini ya asimilia 40.

Katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2023, waliofanya mtihani walikuwa wanafunzi 158 ambapo daraja la kwanza walipata wanafunzi 26, daraja la pili wanafunzi 55, daraja la tatu wanafunzi 35, daraja la nne wanafunzi 42 na hakukuwa na mwanafunzi aliyepata sifuri.

Matokeo haya yanaonyesha wazi kuwa wanafunzi 116 kati 158 watajiunga na kidato tano na vyuo mbalimbali huku shule hiyo kwa shule za serikali ikishika nafasi ya kwanza huku ikishika nafasi ya 9 kwa shule 38 zikiwemo shule za watu binafsi.

Ndemella amesema kwa mwaka 2024 wamejipanga kufanya vizuri zaidi katika ufaulu ambapo ameahidi kuishangaza dunia kuwa Shule ya Sekondari Chifunfu nayo ni miongoni mwa shule bora.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema, Binuru Shekidele amesema ufaulu huu kwa Wilaya ya Sengerema umechangiwa na mshikamano kati ya walimu, wazazi na viongozi wa halmashauri kupokea maelekezo wanayopewa.

Leave A Reply