The House of Favourite Newspapers

Shule ya Sekondari Kingani Yapewa Msaada wa Kuchimbiwa Visima

0

 

Shule ya Sekondari Kingani iliyopo Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, jana imepata faraja kubwa baada kuzinduliwa visima viwili vya maji safi vilivyochimbwa kwa msaada wa Peter Masgen na mkewe Habiba Masgen ambao ni wamiliki wa Kampuni ya MMM ya Ujerumani.

 

Katika uzinduaji wa visima hivyo, Mbunge wa Bagamoyo Muharami Mkenge naye alikuwepo kushuhudia uzinduzi huo, ambapo tatizo la maji maji safi lilikuwa sugu shuleni hapo, kwani wanafunzi walikuwa wakikinga maji yenye kutu kwenye mabati.

Akizungumza mbele ya wanafunzi na watu mbalimbali, Habiba ambaye ni Mtanzania anayeishi nchini Ujerumani, alisema kuwa mkataa kwao ni mtumwa hivyo watu wote wanaoishi nje ya nchi, wakumbuke nyumbani kuna wahitaji wengi.

“Jamani tunawashukuru sana watu wetu tunaoishi nao nje ya nchi kwa kutusaidia katika kupatikana visima hivi viwili, maana tuna ratiba ndefu sana ya kukamilisha visima sehemu nyingi, hivyo niwausie Watanzania wengine wanaoishi nje ya nchi, kukumbuka pia na nyumbani,” alisema Habiba Masgen.

Leave A Reply