The House of Favourite Newspapers

Shule za Feza Kusomesha Wanafunzi Zadi ya Mia Nne (400) Bure

Mkurugenziwa Shule za Feza, Ibrahim Yunus (kushoto) akizungumza na wanahabari.

 

 

Katika kuhakikisha inaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano za kuhakikisha watanzania wanapata elimu bure uongozi wa shule za sekondari  Feza inawadhamini watoto wenye mahitaji wanaosoma katika shule za kata na nyinginezo zilizopo jirani na shule za Feza nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mashindano ya Sayansi yaliyoandaliwa na shule hizo, Mkurugenzi wa  Feza, Ibrahim Yunus alisema.

 

 

“Watoto hawa huchaguliwa na kamati za wazazi na bodi za shule kushirikiana na walimu wao wakuu, ambapo wengi ni yatima, au wanaoishi katika familia zenye mazingira magumu na wanahitaji msaada.

Pamoja na kwamba elimu ni bure, watoto hawa hupatiwa shilingi 250,000 taslimu kila mwaka ili kukidhi mahitaji yao ya madaftari, sare za shule na pesa za matumizi ya siku na mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 400 wamenufaika na ufadhili huo,” aslisema.

 

Miongoni mwa shule ambazo wanafunzi wake ni wanufaika na mpango huo mpaka hivi sasa ni zile zilizopo jirani na Feza ambazo ni, Kawe Ukwamani, Kawe A, Tumaini, Kambangwa, Mikocheni, Kondo, Makongo, Benako, Salasala, Tegeta Pwani,Arusha  na baadhi ya shule za visiwani Zanzibar.

 

Mmoja wa wazazi ambaye mwanaye ni mnufaika wa udhamini huo, Abraham Mwinchande fundi selemala (45) mkazi wa kawe mzimuni alisema anaushukuru uongozi wa shule za feza kwa kuweza kumpatia ufadhili mwanae kwani mwaka huu anaingia kidato cha 3 bila kupata ufadhili huo angekuwa yupo yupo mtaani kwa kuwa mimi baba yake hali ya kipato na badala yake angeishia kuendesha bodaboda.

 

Aidha uongozi wa shule hiyo umewataka wazazi kuwajengea uwezo wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi ili kuweza kupata nafasi ya kusoma bure katika moja ya shule zao.

Ukifatilia matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa hivi karibuni Shule za Feza ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri kitaaluma nchini, ambapo shule mbili za Feza ziliingia katika kumi bora na kutoa wanafunzi 8 ndani ya kumi bora za wanafunzi hali inayoongeza hamasa ya kufundisha na wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuweza kuendelea katika nafasi za juu kitaaaluma.

 

Lakini mbali na taaluma shule yetu ina mpango maalumu wa kusaidia jamii kwa kuchimba visima na kujenga madarasa katika shule mbalimbali.

Comments are closed.