Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji akizungumza jambo katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
Taswira ya ofisi ya spika wakati wa ugeni huo.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (mbele), wakati alipokuwa ofisini kwake leo akikutana na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
MBUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji amempongeza Spika wa Bunge, Job Ndugai, kwa kuchaguliwa kwake kuwa spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa serikali ya awamu ya tano.
Shy-Rose Bhanji ameyasema hayo leo alipowawakilisha wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ofisini kwa spika katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam alipokutana na Ndugai kwa ajili ya kufahamiana na kumpongeza kwa kazi nzuri toka alipokuwa naibu spika wa bunge la awamu ya nne.
Pia Bhanji amempongeza Rais Magufuli kwa kushughulikia kero mbalimbali nchini zikiwemo zinazohusiana na bandari, mambo ambayo Bunge la Afrika Mashariki lilikuwa likiyazungumzia.
Amesema tangu kuingia kwake Ikulu, Rais Magufuli amekuwa akisimamia uchumi wa nchi na kupambana na watu wanaohusishwa na masuala ya ufisadi huku akisema serikali ya awamu ya tano imekuja na mtindo wa kufanya kazi mara moja bila kusubiri.
Stori: Denis Mtima/Gpl