SIFA 10 ZA MUME BORA

 

Imekuwa ni vigumu sana kwa walio wengi kufanya chaguo juu ya mwenzi bora wa kudumu naye, hasa kwa upande wa wanawake/waschana kwenye kutoa maamuzi juu ya wanaume pindi wanapoleta maombi.

 

Unapofanya chaguo lisilosahihi katika mahusiano yako ndivyo unavyo hatarisha amani ya familia yako kwa siku za zijazo.Kuwa makini kwenye kufanya chaguo sahihi.

 

Kwa wewe mwanamke/mschana hii nimeandaa kwaajili yako lakini baada ya kusoma na kuchukua hatua, inakubidi uhakikishe kwamba unachukua muda wa kutosha kuchunguza chaguo lako kwasababu wengi wanavaa ngozi ya kondoo.

 

1Ametulia si macho juu kama nzi, kila akionachi hata kama ni kichafu chaliwa.

 

2.Anajiheshimu, anaheshimu mkwe, ndugu wa pande zote, watu wengine pamoja na majirani.

 

3.Mwenye huruma na mapenzi ya kweli kwa mke na familia kwa ujumla.

 

4.Mtunzaji wa familia na si bahili au mfujaji wa mali.

 

5.Mcha Mungu na mwenye utu.

 

6.Mchapa kazi, asiyekata tamaa, si mvivu na goi goi.

 

7.Msaidizi, sio mke na jembe na kuni, yeye kashika bakora anapunga mkono, shughuli zote za uzalishaji mali na utunzaji wa familia kumuachia mke.

 

8.Mwenye kupenda kujadiliana, sio amri ikitoka imetoka hata kama pumba zenye madhara mradi yeye kasema basi naibaki iwe hivyo.

 

9.Mwenye kutimiza wajibu wake kwenye masuala ya unyumba, sio mume jina, chakula anakula baranarani huku mkewe analala na njaa.

 

10.Mwenye kuona wivu kwa mkewe sio kila mtu basi ruksa kula chakula nyumbani kwake ilimradi yeye kaoa basi kaolea jamaa na marafiki.

 

Loading...

Toa comment