MWANAHERI: SIJAFUATA PESA KWA MUME, NI MAHABA TU!

Yapo mengi ambayo yamezungumzwa kuhusu msanii wa filamu Bongo, Mwanaheri ahmed. Mengine yana ukweli lakini yapo ambayo ni uzushi. Waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta msanii huyu na kufanya naye mahojiano. Fuatilia hapa chini…

 

Mwandishi: Unaonekana kwenye tamthiliya mbili, ile ya Kiu ya Kisasi na sasa mnashuti sehemu ya tatu ya Tamthiliya ya Kapuni, vipi unawezaje kugawa muda wako?

 

Mwanaheri: Unajua Tamthiliya ya Kiu ya Kisasi mara ya kwanza ilikuwa inaonyeshwa Azam Two lakini baadaye ikahamishiwa TBC. Kuhusu kugawa muda, naweza kufanya hivyo kwa sababu Kiu ya Kisasi ilishaisha na sasa ndio tunashuti tamthiliya mpya ya Kapuni.

 

Mwandishi: Kwa nini uliamua kujiingiza kwenye biashara ya kuuza madela? Mwanaheri: Niliamua kujiingiza kwenye biashara hiyo kwa sababu maisha siyo sehemu moja na maisha siyo kitu kimoja, hivyo kama kweli wewe ni mtafutaji huwezi ukabaki unafanya kitu kimoja kila siku. Mwandishi: Una elimu gani?

 

Mwanaheri: Nina digrii ya mambo ya Bima niliyoipata katika Chuo cha IFM. Mwandishi: Ulijisikiaje siku ya kwanza kuambiwa umefanana na Riyama? Na vipi baada ya kufanya naye kazi?

 

Mwanaheri: Nilijisikia vizuri, hata baada ya kufanya naye kazi nilifarijika kwa sababu ni  mtu mzuri asiyependa makuu. Mwandishi: Msanii gani hapa Bongo huwa unajisikia poa kufanya naye kazi?

 

Mwandishi: Kwa kweli mimi huwa nafurahi kufanya kazi na msanii yeyote nitakayepangwa naye. Mwandishi: Msanii gani anakuumiza kichwa kwenye sanaa na unatamani siku moja ufikie levo zake?

 

Mwandishi: Mmh! Hakuna msanii yeyote ambaye ananiumiza kichwa kwenye sanaa yetu, zaidi huwa naumiza kichwa changu mwenyewe, kwa sababu nataka nifike sehemu f’lani. Mwandishi: Kuna tetesi kwamba ulikubali kuolewa na huyo mwanaume kwa sababu ya pesa, hili limekaaje?

 

Mwanaheri: (Anacheka) Tetesi za kuolewa kwa sababu ya pesa siyo za kweli. Unajua yule mwanaume siyo kipofu, ameona wanawake wangapi mpaka aje kwangu? Kwa hiyo alinipenda na mimi nikampenda ndio maana mpaka sasa tupo pamoja.

 

Mwandishi: Vipi maisha ya ndoa, unayaonaje? Mwanaheri: Maisha ya ndoa ni matamu kwa kweli, kama unapenda na wewe unapendwa basi hatajutia, namshukuru Mungu kwa hilo. Mwandishi: Ni muda mrefu kidogo umepita tangu uingie kwenye ndoa, vipi hili la kuitwa mama?

Mwanaheri: Napenda sana watoto na mpaka sasa sina mtoto, japo wapo watoto wa ndugu zangu ambao nawapenda kama wanangu na wao wananichukulia kama mama yao. Mimi kwa kweli natamani kuitwa mama hata leo na kwa kuwa ni suala la majaaliwa ya Mungu, naamini ipo siku ndoto hiyo itatimia.

 

Mwandishi: Umewahi kufanya muziki? Mwanaheri: Sijwahi kuingia kwenye muziki na wala sifikirii kufanya muziki. Mwandishi: Mwanaheri ni mtu wa aina gani?

 

Mwanaheri: Mimi ni mtu ambaye napenda sana kufurahi na napenda kuwa na amani wakati wote, pia ni mtu ambaye napenda hata watu wanaonizunguka wawe na furaha ndio na yeye anafurahi.

 

Mwandishi: Umeshawahi kutamani kupungua mwili? Mwanaheri: Yaani sijawahi kutamani kupungua mwili wangu, ila nimewaza kupungua tumbo tu. Mwandishi: Ujumbe kwa wananzengo ambao wanadai umefuata pesa kwa mumeo.

 

Mwanaheri: Ujumbe ninawaambia kwamba pesa kila mtu anazihitaji. Hivyo kama mimi nimefuata pesa kwa mume wangu, na wao kwa nini hawawafuati hao watu wenye pesa? Mbona matajiri wapo wengi tu mjini hapa?

MAUNO YA PAM D NDANI YA STUDIO ZA 255 GLOBAL RADIO


Loading...

Toa comment