Nandy: Sijawahi Kuonja Kofi la Billnass

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya, Faustina Mfinanga ‘Nandy’ ameutupilia mbali uzushi unaodai kuwa mara nyingi anapata kipigo kutoka kwa mchumba wake William Lyimo ‘Billnass’ na kusema kuwa hajawahi hata kuonja kofi lake.

 

Akizungumza na AMANI, Nandy alisema mchumba wake huyo ni mwanaume mpole na hata hadhani kabisa anaweza akampiga mtu yeyote kwa maana hata yeye hajui kofi lake.

 

“Jamani sidhani kabisa kama Bill, anajua hata kugombana na mtu na kingine tangu namfahamu hajawahi hata kunipiga kofi, sasa huyo anayesema ananipiga, sijui anataka nipigwe kweli,” alisema Nandy huku akicheka.

 

Mwanamuziki huyo hivi karibuni alifungua ofisi yake mpya inayoitwa Nandy Bridal, ambayo itakuwa ikijihusisha na mambo yote ya sherehe mbalimbali.

Stori: Imelda Mtema

Toa comment