The House of Favourite Newspapers

Sijibomi: Bilionea Kijana Mwenye Akili ya Biashara

0


MAKALA: NYEMO CHILONGANI | IJUMAA WIKIENDA | UTAJIRI

HEBU jaribu kujifi kiria, leo umefi kisha umri wa miaka 33. Bado unafi kiria kuhusu elimu yako. Ni kwa jinsi gani utaendelea kusoma mpaka upate ‘masta’ yako na kuajiriwa. Wakati huohuo, kuna kijana nchini Nigeria ni bilionea, tena akiwa katika umri kama wako.

Unaweza kuhisi Mungu amekuonea! Ndugu yangu, Mungu hamuonei mtu, yeyote ambaye atajituma kwa nguvu zote ni lazima atafanikiwa. Hakuna jasho linalokwenda bure. Kama unakesha ukisoma, hakuna usingizi unaokwenda bure. Kama unaamka mapema kuwahi kazini, jua kwamba hakuna muda unaokwenda
bure.

Unapozungumza mabilionea vijana barani Afrika, basi utakuwa umefanya kosa kubwa kama hutalitaja jina la bilionea Sijibomi Ogundele, Mnigeria anayetikisa kwa utajiri mkubwa. Ni miongoni mwa vijana wenye utajiri mkubwa barani Afrika.

Ni akili tu ndiyo iliyomfanya kuwa hapo alipo kiasi kwamba mpaka mtandao wa mabilionea, Forbes ukamchagua kama bilionea kijana mwenye akili anayesababisha mabadiliko mengi nchini Nigeria.

AJENGA APATIMENTI YA GHARAMA NIGERIA

Jamaa huyu siyo mtu wa mchezomchezo kwani amejenga apatimenti za gharama kubwa nchini Nigeria ambazo zipo katika Mtaa wa Ikoyi huko Lagos. Jamaa hajishughulishi na ishu hiyo tu, bali ana kampuni za mafuta nchini Nigeria huku akiwa na ofi si zake Paris nchini Ufaransa, Accra, Ghana, Madrid nchini Hispania, Dubai na Rihadh huko Falme za Kiarabu. Mbali na hayo yote, pia ana kampuni yake ya ujenzi ya Sujimoto ambayo imekuwa ikijenga majengo mengi duniani.

AFANYA KAZI UARABUNI
Mbali na kufanya kazi na makampuni mengi barani Afrika, pia ameamua kufanya kazi na makampuni mengi duniani kama Fortune 100 Alhaji Group ambayo inajulikana kama moja ya kampuni kubwa huko Uarabuni.

ANUNUA SAA SH.
MILIONI 300 Pamoja na utajiri mkubwa alionao, Sijibomi anasema kwamba amekuwa mtu wa kuishi maisha ambayo yanamfanya kujua kwamba yeye ni bilionea. Si mtu wa kujivunga kwani aliutafuta ubilionea ili aishi maisha mazuri hivyo akaamua kununua saa kwa dola 150,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 300.

…Akiwa na bilionea Al-Haji Aliko Dangote.

UTAJIRI WA BILIONI 2.5
Leo, Sijibomi ana utajiri mkubwa wa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 huku akiendelea kuwekeza kila siku kiasi kwamba watu wengi wanamtabiria kuwa na utajiri mkubwa hata zaidi ya bilionea namba moja Afrika, Mnigeria mwenzake, Aliko Dangote hapo baadaye.

SI MTU WA MAJIVUNO
Miongoni mwa mabilionea ambao wanaonekana kuwa simpo basi kwa Afrika, Sijibomi anaweza kushika nafasi ya kwanza. Si mtu wa kujiona, amekuwa mtu wa kusaidia watu wengi ambao wapo kwenye maisha duni nchini Nigeria.
Ni mtu wa kujichanganya na watu wengine na mara nyingi amekuwa akitembelea mitaa ya kimaskini nchini humo.

BILIONEA MWENYE AKILI
Kati ya matajiri wenye akili nchini Nigeria, yeye ni miongoni mwa watu hao. Amekuwa mbunifu katika biashara nyingi anazozifanya. Amekuwa akianzisha biashara mbalimbali kwa haraka sana.

Alipoona kwamba Nigeria ina mafuta mengi, akaamua kuungana na kampuni kadhaa za mafuta katika Falme za Kiarabu ili kuuongeza utajiri wake kwani aligundua kwamba huwezi kufanya biashara ya mafuta kama hutaweka uswahiba mzuri na Waarabu ambao mafuta yao yamekuwa na thamani kubwa duniani kwa sasa.

VIPI KUHUSU WEWE?
Wengi wanahisi kwamba utajiri ni bahati! Hapana, utajiri si bahati bali ni matokeo ya mambo uliyokuwa ukiyafanya. Huwezi kutajirika kama hujitumi. Huwezi kutajirika kama siyo mtu wa kujiwekea malengo.
Mara zote watu wanaofanikiwa ni wale wanaojituma. Huwezi kukaa chumbani, hutoki halafu useme fedha zitakufuata kwa kuwa umeandikiwa utajiri.

Mbali na kujituma, ni lazima uwe mbunifu sana katika biashara zako. Hazitakiwi ziwe kama zilivyokuwa mwaka jana. Kama ni chakula ni lazima kibadilike ladha, kama ni biashara nyingine ni lazima ziwe na muonekano mwingine. Hiyo itawafanya watu kutokukuchoka, itawafanya watu kutamani kuwa na bidhaa zako kila siku.

Leave A Reply