The House of Favourite Newspapers

Siki ya tufaha hutibu harufu mwilini

0

BLD080939

WATU wengi wamekuwa wakinilalamikia kusumbuliwa na harufu mwilini, hii hapa ni tiba ya tatizo hilo, kwa wenye uwezo wanaweza kuitumia kwa kuoga mara moja au mbili kwa wiki, nasema uwezo kwa sababu si rahisi sana kuipata, kwani inauzwa katika maduka makubwa ya vyakula.

Jinsi ya kuoga

Chukua kikombe kimoja au viwili vya Siki ya Tufaha ‘Apple’ weka kwenye maji ya moto au vuguvugu kisha acha kwa muda wa dakika 20 au 30, baada ya hapo chukua nguo iloweke na ujisugulie mwilini. Kama sehemu zinazotoa jasho baya, unaweza kuosha kwa maji hayo kwanza kisha ndiyo usugue na kitambaa unachotumia, mfano kwapani, kwenye vidole na pembeni mwa mapaja.

Baada ya hapo acha maji yake yaliyochanganywa na siki yakauke mwilini ili kukusaidia kuondoa harufu hiyo.

Siki hii imekuwa ikitumika kutibu vitu vingi, mbali na kukuondolea jasho mwilini pia husaidia kuifanya ngozi yako kung’aa na kuwa na muonekano mzuri.

Leave A Reply